Pata taarifa kuu
UJERUMANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Maambukizi ya virusi vya Corona yapindukia watu 156,000 Ujerumani

Idadi ya visa vipya vilivyothibitishwa vya maambukizi ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 nchini Ujerumani imepanda hadi 156,337.

Tangu Jumatatu, Aprili 27, kuvaa mask ni lazima nchini Ujerumani, katika sekta ya uchukuzi na karibu kila mahali katika maduka. Hapa bi katika mji wa Bad Badnef, karibu na Bonn.
Tangu Jumatatu, Aprili 27, kuvaa mask ni lazima nchini Ujerumani, katika sekta ya uchukuzi na karibu kila mahali katika maduka. Hapa bi katika mji wa Bad Badnef, karibu na Bonn. REUTERS/Wolfgang Rattay
Matangazo ya kibiashara

Ugonjwa wa Covid-19 sasa umesababisha vifo vya watu 5,913 nchini, kulingana na takwimu zilizotolewa leo Jumanne na Chuo Kikuu cha Marekani cha Robert Koch (RKI).

Hii inonesha visa vipya 1,144 vya maambukizi, sawa na kupungua kwa idadi ya kila siku baada ya kuongezeka siku tatu mfululizo, na vifo vipya 163 ndani ya masaa ishirini na nne, kulingana na ripoti ya RKI.

Rekodi mpya ya visa vya maambuziki ya virusi vya Corona hadi sasa inaonesha vimepindukia watu milioni tatu duniani kote, ambapo karibu asilimia 80 vimerekodiwa Ulaya na Marekani.

Kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP takribani maambukizi 3,003,344 yamebainika, ikiwemo vifo 209,388, na vingi vya hivyo vimetokea Ulaya ambako kuna jumla ya maambukizi 1,393,779 na vifo 126,233. Marekani kuna maambukizi 980,008 vikiwemo vifo 55,637.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.