Pata taarifa kuu
DUNIA-WHO-CORONA-AFYA

Viongozi wa dunia wafanya jitihada za kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19

Shirika la afya duniani WHO linasema rais wa Ufaransa Emanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel wanaungana pamoja kuzindua mpango wa kusaidia kupatikana kwa dawa  na chanjo dhidi ya maambukizi ya Corona.

Ugonjwa wa Covid umesababisha vifo vya watu wengi dunia.
Ugonjwa wa Covid umesababisha vifo vya watu wengi dunia. AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa WHO Fadela Chaib amesema mpango huo wa kihistoria utawekwa wazi baadaye siku ya Ijumaa, ili kuharakisha jitihada za kupata chanjo na dawa dhidi ya virusi hivyo vinavyoendelea kuitesa dunia.

Ripoti zinasema kuwa mbali na viongozi hao wa Ufaransa na Ujerumani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus watashuhudia uzinduzi wa jitihada hizo ambazo wengi wanaona ni mshirikamano wa pamoja wa kisiasa.

Hadi sasa inaripotiwa kuwa wanasayansi wanajaribu kutengeza chanjo zaidia ya 100 katika maabara mbalimbali duniani na tayari chanjo sita zipo majaribuni.

Kufanikiwa kupata chanjo au dawa dhidi ya virusi vya Corona, utakuwa ni ushindi mkubwa dhidi ya ugonjwa huu ambao umewaambukiza watu zaidi ya Milioni 2.7 na kusababisha vifo vya watu wengine zaidia ya 190,000 kote duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.