Pata taarifa kuu
UJERUMANi-UCHUMI

Almasi "zenye thamani isiyojulikana" zaibwa katika jumba la makumbusho Ujerumani

Vito vitatu vya almasi vya karne ya 18 "vyenye thamani isiyojulikana" vimeibiwa katika jumba la makumbusho katika mji wa Dresden, nchini Ujerumani. Jumba hili lina mkusanyiko wa hazina wa kipekee barani Ulaya.

Jumba la makumbusho la Dresden, ambapo almasi zenye thamani isiyojulikana zimeibiwa, Novemba 25, 2019.
Jumba la makumbusho la Dresden, ambapo almasi zenye thamani isiyojulikana zimeibiwa, Novemba 25, 2019. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumatatu alfajiri, wezi wawili wamefanikiwa kuingia ndani ya jumba la makumbusho la "The Green Vault", ambalo lina sehemu 4,000, na kuweza kuiba vito vitatu vya almasi na mali nyingine, kwa mujibu wa polisi.

"Tunasikitishwa na uhalifu huu," Mkurugenzi wa jumba la Makumbusho, Marion Ackermann amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Marion Ackermann amezungumzia kuhusu kupotea kwa vito vyenye thamani ya kihistoria na kiutamaduni "isiyoweza kujulikana" na isiyoweza kuhesabilika. "Hatuwezi kusema thamani ya vito hivyo kwa sababu sio ya kuuza," Ackermann ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.