Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO-SIASA

Johnson ataka uchaguzi wa mapema kufanyika Oktoba 15

Boris Johnson ameanza mvutano mpya na Bunge la Uingereza leo Jumatano (Septemba 4) siku mojs baada ya kupata pigo kubwa kuhusu mpango wake wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya bila ya mkataba Jumanne wiki hii.

Waandamanaji wabaopinga Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, wakiandamana mbele ya Bunge Westminster, Septemba 4, 2019.
Waandamanaji wabaopinga Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, wakiandamana mbele ya Bunge Westminster, Septemba 4, 2019. REUTERS/Henry Nicholls.
Matangazo ya kibiashara

Johnson amesema angali ana imani kuwa viongozi wa Umoja wa Ulaya watakubaliana kuondoa kipengee chenye utata kuhusu mpaka wa Ireland maarufu kama “backstop” kwenye makubaliano yao.

Kipengee hicho kinalenga kuweka wazi mpaka kati ya Ireland kaskazini na jamhuri ya Ireland baada ya Brexit.

Wabunge wanatarajiwa kupiga kura kuhusu sheria inayolenga kuzuia Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya bila ya mkataba, kama anavyopendekeza waziri mkuu.

Ikiwa wabunge watapiga kura kwa kuzingatia sheria hii, yaani dhidi ya mpango wa serikali, Boris Johnson amesema atawasilisha hoja kwa Baraza la wawakilishi kuitisha Uchaguzi Mkuu mapema Oktoba 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.