Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA-USALAMA

Macron kulihutubia taifa Jumatatu hii

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kulihutubia taifa baadae Jumatatu hii, April 15 jioni, ambapo maswala kuhusu muendelezo wa mjadala wa kitaifa ulioandaliwa ili kutafuta suluhu ya mzozo wa waandamanaji wenye vizibao vya njano uliodumu sasa ni miezi mitano yataangaziwa.

Emmanuel Macron, Aprili 4, 2019, Cozzano (Corse-du-Sud) kwa mjadala wa mwisho wa kitaifa.
Emmanuel Macron, Aprili 4, 2019, Cozzano (Corse-du-Sud) kwa mjadala wa mwisho wa kitaifa. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baadae Jumatano Emmanuel Macron pia atajibu maswali ya waandishi wa habari.

Emmanuel Macron anaelekea kutekeleza ahadi yake kuhusu mjadala, hitimisho la mjadala wa kitaifa, ambapo inatarajiwa kuwa katika hotuba yake ya Jumatatu hii jioni ataweka wazi mipango yake iliopewa kipao mbele pamoja na hatua halisi za kwanza kukabiliana na masuala yaliyotolewa katika mazingira ya mjadala mkubwa wa taifa.

Rais Macron ameamuwa kuweka kipao mbele kwa kuzungumza moja kwa moja na wananchi wa Ufaransa, lakini pia amepanga kujibu maswali ya waandishi wa habari, ikiwa ni mkutano wake wa kwanza wa aina hiyo katika kipindi hiki ambapo atajibu maswali yote na kuyatolea maelezo ya kina.

Haya ni mabadiliko ya mfumo kutokana na kwamba mjadala mkubwa wa kitaifa ni dhahiri ni wakati muhimu kwa rais ambae anataka mabadiliko katika msimu huu wa uongozi ili kuufunga ukurasa wa waandamanaji wenye vizibao vya njano.

Hata hivyo hakuna kilichochomoza katika hatua ambazo zinatarajiwa kuchukuliwa na rais Macron ispokuwa tu mitazamo ya watu kwamba huenda hatua zikachukuliwa kuhusu uwezo wa ununuzi kwa manufaa ya wastaafu, familia zenye kuwa na mzazi moja, lakini pia hatua za kuboresha utendaji wa kidemokrasia au kukuza mabadiliko ya ulinzi wa mazingira, pamoja na hatua zote kuhusu kodi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.