Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAJANGA

Ufaransa: Saba wapoteza maisha katika mkasa wa moto Paris

Watu saba wamepoteza maisha katika mkasa wa moto uliozuka katika jengo moja jijini Paris, nchini Ufaransa, usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne hii, Februari 5, 2019.

Kikosi cha Zima Moto kikiendelea na shughuli ya uokoaji katika wilaya ya 16 Paris, Jumanne, Januari 5.
Kikosi cha Zima Moto kikiendelea na shughuli ya uokoaji katika wilaya ya 16 Paris, Jumanne, Januari 5. Geoffroy VAN DER HASSELT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Pia watu kadhaa wamejeruhiwa katika mkasa huo, ikiwa ni pamoja na mmoja ambaye yuko katika hali mbaya.

"Idadi hiyo inaweza kuongezeka kwa sababu moto huo bado unaendelea kwenye ghorofa ya 7 na ya 8," amesema msemaji wa kikosi cha Zima Moto.

Sababu za moto huo bado hazijajulikana.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa, moto huo ambao umezuka katika jengo la wilaya ya 16 ya mji mkuu wa Ufaransa karibu saa 7 usiku (saa za Paris), umeua watu saba, na kujeruhi watu 27, ikiwa ni pamoja na maafisa watatu wakikosi cha Zima Moto, huku mtu mmoja akiwa katika hali mbaya.

Zoezi la uokoaji bado linaendelea kwa mujibu wa Cognon, msemaji wa kikosi cha Zima Moto akihojiwa na shirika la Habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.