Pata taarifa kuu
UFARANSA-MOTO-MAZINGIRA

Zaidi ya ekari 7,000 zateketea kwa moto kusini mwa Ufaransa na Corsica

Moto wa nyika unaoendelea nchini Ufaransa tayari umeharibu zaidi ya hekta 7,000 kusini mwa nchi hiyo na Corsica. Zaidi ya watu 10,000 walihamishwa siku ya Jumatano usiku kutaoak wilaya ya Bormes-les-Mimosas, katika eneo la Var, eneo la kitalii.

Watu wengi walihamishwa kutoka wilaya ya Bormes-les-Mimosas, siku ya Jumatano, Julai 26, 2017.
Watu wengi walihamishwa kutoka wilaya ya Bormes-les-Mimosas, siku ya Jumatano, Julai 26, 2017. REUTERS/Jean-Paul Pelissier
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya watu wanatazaiwa kulala nje kutokana na hali hiyo inayoendelea. Waziri Mkuu Edouard Philippe alisafiri kwa ndege kujionea mwenye hali hiyo.

Moto huo kwa sasa unaelekea eneo jingine la Bormes-les-Mimosas, ambapo wakazi wake wanatazamiwa kuondoka jioni au usiku.

Wazima moto wametumwa kupambana na moto huo karibu na maeneo la Bormes-les-Mimoses.

Mapema Ufaransa iliiomba majirani wake wa EU msaada zaidi kupambana na moto huo.

Karibu ekari 4,000 za ardhi zimeteketea katika pwani ya Mediterranean.

Katika eneo la Corsica mamia ya nyumba zimehamwa.

Kwa ujumla wazima moto 400 na wanajeshi wanaotumia maji wanajaribu kuuzima moto huo tangu siku ya Jumatatu.

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, takriban wazima moto 12 wamejeruhiwa na polisi 15 kuathiriwa na moshi kutokana na moto huo.

Moto wa nyika walazimu maelfu kuhamishwa Ufaransa.
Moto wa nyika walazimu maelfu kuhamishwa Ufaransa. REUTERS/Jean-Paul Pelissier

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.