Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFYA-ELIMU

Emmanuel Macron afafanua sera yake ya uongozi

Siku ya Jumatatu rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alifafanua katika baraza la seneti hatuwa kadhaa katika sera yake ya uongozi wa Wilaya za nchi hiyo.

Emmanuel Macron wakati wa Mkutano wa kitaifa kuhusu wilaya, Julai 17, 2017, Paris.
Emmanuel Macron wakati wa Mkutano wa kitaifa kuhusu wilaya, Julai 17, 2017, Paris. REUTERS/Ian Langsdon
Matangazo ya kibiashara

rais Macron alisema ataongeza mara mbili idadi ya Hospitali, kukomesha kufungwa kwa madarasa ya vijijini, kuongeza uwezo zaidi ya upokeaji wa Internet katika wilaya zote za nchi mwaka 2020 badala ya 2022 kama ilivyoahidiwa hapo awali.

Hatua hizo zimepokelewa kwa mtazamo chanya na wajumbe wa baraza la seneti. Hata hivyo wajumbe hao hawakubaliani na mpango wa rais Macron wa kupunguza idadi ya madiwani wa ndani, hatua ambayo ilitangazwa hapo awali na Waziri wa Bajeti Gérald Darmanin kabla ya kuthibitishwa na rais Macron

Rais Macron alisema serikali za mitaa zitakuwa na bilioni 13 katika akiba kwa kipindi cha miaka mitano, ikiwa ni zaidi ya bilioni 3 kama ilivyotangazwa wakati wa kampeni za uchaguzi. Rais Macron amesisitiza lengo lake la kuondoa kodi ya makazi kwa 80%.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.