Pata taarifa kuu
UFARANSA-JESHI

Mkuu wa Majeshi nchini Ufaransa ajiuzulu

Mkuu wa majeshi nchini Ufaransa Jenerali Pierre de Villiers amejiuzulu.

Mkuu wa Majeshi nchini Ufaransa Jenerali Pierre de Villiers aliyejiuzulu.
Mkuu wa Majeshi nchini Ufaransa Jenerali Pierre de Villiers aliyejiuzulu. REUTERS/Stephane Mahe/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Villiers amesema amechukua hatua hiyo baada ya kutofautiana na rais Emmanuel Macron kuhusu kupunguza bajeti ya wanajeshi.

Aidha, amesema kuwa ameamua kuondoka kwa sababu hawezi kuthibitisha iwapo jeshi hilo litaendelea kuwa imara ikiwa bajeti hiyo itapunguzwa.

Wiki iliyopita, serikali ya rais Macron ilitangaza kuwa ilikuwa na mpango wa kupunguza bajeti hiyo ili kuwa chini ya kiwango kinachopendekezwa na Umoja wa Ulaya angalau kwa asilimia tatu.

Hata kabla ya kujiuzulu kwa Jenerali Villiers, rais Macron alinukuliwa na Jarida la du Dimanche akisema hatakubali uamuzi wake kutotekelezwa na kumtaka Mkuu wa jeshi hataki kushirikiana naye, basi aondoke.

Serikali ya Ufaransa imesema itapunguza bajeti ya jeshi kwa Euro Milioni 752 mwaka 2017.

Jeshi la Ufaransa kwa miaka mingi limefahamika kushirikiana na mataifa mengine ya Kimataifa katika operesheni nje ya nchi hiyo lakini pia kusaidia kupambana na makundi ya waasi na kigaidi nchini Mali na Jamhuri ya Afrika ya Kati barani Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.