Pata taarifa kuu
UFARANSA-IRAQ-ISIL-Usalama

Iraq: jeshi la Ufaransa laendesha mashambulizi dhidi ya IS

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa amesema jeshi la Ufaransa limeendesha mashambulizi ya anga dhidi ya ngome za wapiganaji wa kundi la Dola la Kiislam nchini Iraq. Operesheni hiyo, ambayo Jean-Yves Le Drian amesema ni muhimu yemeendeshwa Ijumaa Desemba 5 mapema asubuhi.

Mirage 2000D ni moja ya ndege za jeshi la Ufaransa ambazo zinaendesha mashambulizi katika ardhi ya Iraq.
Mirage 2000D ni moja ya ndege za jeshi la Ufaransa ambazo zinaendesha mashambulizi katika ardhi ya Iraq. AFP PHOTO / PASCAL GUYOT
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo ambaye hakutoa taarifa zaidi kuhusi idadi ya ndege za Ufaransa ambazo ziliendesha mashambulizi hayo. Mashambulizi ya leo ni ya 120 tangu Ufaransa ianzishe mashambulizi nchini Iraq mwezi Septemba mwaka 2014.

“ Kuna mashambulizi ambayo yameendeshwa mapema leo asubuhi, lakini si mara ya kwanza jeshi la Ufaransa linaendesha mashambulizi dhidi ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam”, amesema Jean-Yves Le Drian wakati alipokua akihojiwa na kundi la vituo vya redio na televisheni vya BFM-TV-RMC.

“ Mashambulizi ya leo ni sehemu ya mashambulizi yaliyokua yakitekelezwa mara kwa mara na muungano wa kimataifa. Lengo letu au la muungano, nchini Iraq ni kufanya msaada wa mashambulizi ya angani yanayohitajika. Kila siku, tunapiga doria ya kutambua maeneo ambayo yanatakiwa kulengwa na mashambulizi yetu, na kila siku tunafaulu katika mashambulizi yetu", ameongeza Le Drian.

Waziri Le Drian amebaini kwamba operesheni hiyo inaendeshwa kwa ustadi mkubwa, lakini suala hili litachukua muda mrefu, kwa sababu ni lazima kwanza kuruhusu vikosi vya Iraq viweze kujiunga pamoja. Pia kuruhusu vikosi hivyo pamoja nawapiganaji wa kikurdi kuweka kwenye himaya yao hatua kwa hatua maeneo waliyopoteza.

" Yote hii kwa msaada wa muungano huo, lakini bila ya kuwepo kwa majeshi yetu ya ardhini", amesema Le Drian.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.