Pata taarifa kuu
UFARANSA-IS-MAREKANI-SYRIA-MAUAJI-HAKI ZA BINADAMU

Maxime Hauchard, raia wa Ufaransa katika IS

Maxime Hauchard, anasadikiwa kuwa mmoja kati ya wapiganaji wa Dola la Kiislam ambao walionekana katika video iliyorushwa hewani Jumapili Novemba 16 wakati walipokua wakiwakata vichwa wanajeshi wa Syria.

Maxime Hauchard. Picha yake ilirekodiwa kupitia video iliyorushwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, Jumapili Novemba 16 mwaka 2014.
Maxime Hauchard. Picha yake ilirekodiwa kupitia video iliyorushwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, Jumapili Novemba 16 mwaka 2014. DR
Matangazo ya kibiashara

Maxime Hauchard, mwenye umri wa miaka 22, mkaazi wa Normandie nchini Ufaransa, alibadili dini na kuwa muislam akiwa na umri wa miaka 17.

Serikali ya Ufaransa imethibitisha kuwa raia huyo wa Ufaransa ni miongoni mwa wapiganaji wa Dola la Kiislam walioonekana katika video iliyorushwa na kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam Jumapili Novemba 16.

Baada ya kubadili dini na kuwa muislam Maxime Hauchard  alibadili pia jina, na kwa sasa anaitwa Abou Abdallah al Faransi.

Maxime Hauchard alijielekeza nchini Syria mwezi Agosti mwaka 2013, baada ya kuishi nchini Mauritania mwaka 2012, amesema waziri wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve, katika mkutano na vyombo vya habari.

Maxime Hauchard pamoja na wapiganaji wenzake wanaendesha harakati zao katika mji wa Raqqa, makao makuu ya kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam, nchini Syria. Alionekana mara kadhaa akishikilia silaha kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, hususan Facebook.

Waziri wa mambo ya ndani, Bernard Cazeneuve, ametolea wito vijana hasa ambao wamekua wakilengwa na propaganda za kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislam. Bernard Cazeneuve amewataka viajana kutokubali kujiunga na watu ambao amewaita “wahubiri wa chuki”.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.