Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAJANGA

Moto mkubwa kusini mwa Ufaransa, wakazi wahamishwa Vitrolles

Moto mkubwa umezuka kaskazini mwa mkoa wa Marseille. Maafisa 1,500 wa kitengo cha Zima Motowalitumwa Jumatano usiku kujaribu kuzima moto huo. Moto huo ambao kwa sasa umeendelea kushika kasi, tayari umeteketeza hekta 2,700.

Baadhi ya wakazi wanaagalia, wengine wakikimbia moto ambao tayari umeteketeza hekta 200 katika mji wa Vitrolles, Agosti10, 2016.
Baadhi ya wakazi wanaagalia, wengine wakikimbia moto ambao tayari umeteketeza hekta 200 katika mji wa Vitrolles, Agosti10, 2016. BORIS HORVAT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Nyumba zisizopungua 25 pia zimeteketezwa kwa moto. Moto huo umesababishwa na ukame kusini mwa Ufaransa, ambapo kunashuhudiwa upepo hasa mkali. Wakazi wa maeneo kadhaa katika mji wa Vitrolles, mji unaopatikana kilomita thelathini kutoka mkoa wa Marseille, wamehamishwa.

Moto huo tayari umekaribia mji huo katika meneo mengi kadhaa, huku moshi ukifumba na kulivamia eneo jirani.

Wakazi wengi wa mji huo wamesea kuwa na wasiwasi kwamba huenda mali zao zikateketezwa kabisa na moto huo.

Malfu ya raia kwa ujumla wamehamishwa katika mji wa Vitrolles kwa haraka.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Bernard Caseneuve, alijielekeza jana usiku kwenye makao makuu ya kitengo cha Idara ya dharura, katika mjini Aix-en-Provence. Lengo ni kuzuia moto huo kuvamia miji kadhaa, ikiwa ni pamoja na Marseille, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ufaransa, waziri Cazeneuve amesema.

Moto mwingine, wakati huu unaoshuhudiwa katika eneo la Hérault, kaskazini mwa mji wa Béziers, tayari umeteketeza hekta 200 hekta.Maafisa wanne wa kitengo cha Zima Moto waliokua wakikabiliana dhidi ya moto wamejeruhiwa wakati ambapo moto ulikua ulizingira gari yao. Watatu miongoni mwa maafisa hao wako katika hali mbaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.