Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Uhispania yafuta waranti wa kukamatwa dhidi ya Carles Puigdemont

Jaji wa Mahakama Kuu ya Uhispania Pablo Llarena ameondoa hati ya Ulaya ya kukamatwa iliyotolewa dhidi ya aliyekuwa rais wa Catalonia Carles Puigdemont na wasaidizi wake wanne, vyombo vya habari vya Uhispania vimearifu leo Jumanne.

Aliekua kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont.
Aliekua kiongozi wa Catalonia Carles Puigdemont. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

"Uchunguzi unaonyesha kuwa walitaka kurudi nchini Uhispania," Bw Llarena amesema. Uamuzi kuhusu hati iliyotolewa dhidi Carles Puigdemont na mawaziri wa zamani Antonio Comin, Lluís Puig, Meritxell Serret na Clara Ponsati, ambao walikimbilia nchini Ubelgiji tarehe 30 Oktoba, umewasilishwa kwa mahakama ya Ubelgiji.

Hata hivyo, jaji Llarena ameendelea kushikilia waranti wa kukamatwa nchini Uhispania dhidi ya watuhumiwa watano na wanaweza kukamatwa baada ya kurejea nchini Uhispania , vyanzo vya mahakama vimeeleza.

"Watuhumiwa wanaonekana kuwa walikua na nia nzuri ya kurudi Uhispania ili kushikilia nafasi kadhaa katika uchaguzi wa eneo hilo uliopangwa kufanyika Desemba 21", amebaini Bw Llarena.

Siku ya Jumatatu, wanasheria wa upande wa utetezi walidai kwamba Mahakama ya Ubelgiji haina mamlaka ya kuwahukumu watuhumiwa kwa mashtaka dhidi yao. "Kama wangelitumwa kungelikua na ukiukwaji mkubwa wa haki za msingi", wanasheria Marchand na Bekaert.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.