Pata taarifa kuu
CATALONIA-UHISPANIA-HAKI

Makamu wa rais wa zamani wa Catalonia kuendelea kuzuiliwa

Mahakama Kuu ya Uhispania, leo Jumatatu imekataa kumuachia kwa dhamana aliyekuwa makamu wa rais Catalania Oriol Junqueras, pamoja na waziri wa zamani Joaquim Forn na viongozi wa mashirika mawili yanayotetea uhuru wa Catalonia, ANC na Omnium Cultural.

Aliekua makamu wa rais wa Catalonia Oriol Junqueras (katikati) na mwenzake wa chama cha "Junts pel Si" Marta Rovira (kushoto), washirika wa uchaguzi wa kikanda wa Desemba 21. Hapa, ilikua Oktoba 14, 2017 Barcelona.
Aliekua makamu wa rais wa Catalonia Oriol Junqueras (katikati) na mwenzake wa chama cha "Junts pel Si" Marta Rovira (kushoto), washirika wa uchaguzi wa kikanda wa Desemba 21. Hapa, ilikua Oktoba 14, 2017 Barcelona. PAU BARRENA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa mashirika hayo Jordi Sanchez na Jordi Cuixart, wanashutumiwa uasi na uchochezi.

Mawaziri wa zamani wengine sita, waliowekwa kizuizini kwa kusubiri uchunguzi ukamilike kuhusu tangazo la uhuru wa eneo hilo waliachiwa kwa dhamana ya euro 100,000.

Tangazo la uhuru lililotolewa na serikali ya Catalonia Oktoba 27 limesababisha serikali kuu ya Uhispania kutwaa mamlaka yote ya eneo hilo na imeitisha kura ya mapema tarehe 21 Desemba.

Wajumbe nane wa zamani wa serikali ya Catalonia walilikwa kizuizini Novemba 2 kwa kosa la uasi na ubadhirifu. Wanaomba kuachiliwa kwa dhamana ili waweze kushiriki katika kampeni hiyo.

Rais wa zamani wa Catalania Carles Puigdemont na wanachama wanne wa baraza la mawaziri walikimbilia Ubelgiji. Waranti za kukamatwa dhidi yao na mahakama ya Ubelgiji wamewachia huru kwa dhamana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.