Pata taarifa kuu
EU-USHIRIKIANO

Viongozi wa EU kujadili mpango mkuu wa Macron

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani wanatarajiwa kukutana kabla kuanza kwa mkutano wa Umoja wa Ulaya nchini Estonia.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) katika mkutano wa waandishi wa habari kando ya mkutano wa Umoja wa Ulaya, Brussels, Ubelgiji, tarehe 23 Juni 2017.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel (kushoto) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) katika mkutano wa waandishi wa habari kando ya mkutano wa Umoja wa Ulaya, Brussels, Ubelgiji, tarehe 23 Juni 2017. REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Mkutano huu unakuja baada ya Macron wiki hii kutoa dira yake kuhusu namna ya kuimarisha Umoja wa Ulaya, lakini pia baada ya Kansela Merkel kushinda tena Uchaguzi nchini Ujerumani.

Viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa pia kujadili na kutoa maoni yao kuhusu hatima ya Umoja huo.

Wiki hii Rais Wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa mapendekezo yake katika nyanja mbalimbali ili kufufua mpango wa Ulaya.

Kwenye nyanja ya ulinzi na usalama, Rais Emmanuel Macron, alitoa wito wa kutaka kubuniwa kikosi cha pamoja cha jeshi kama sehemu ya maono yake ya siku za usoni kwa muungano huo.

Bwana Macron alipendekeza kuwa kikosi hicho kipya kitakuwa ni sehemu ya Nato.

Rais Emmanuel Macron alisema anataka mungano wa Ulaya kuboresha mifumo yake ya ulinzi kwa kubuni jeshi la pamoja.

Kwenye nyanja ya uhamiaji, Rais Macron alisema "mgogoro wa wahamiaji ni changamoto ya kudumu. Tunakosa uwezo na ubinadamu, "alisema Emmanuel Macron. Ili kurekebisha hali hii, alipendekeza kuundwa kwa ofisi ya hifadhi ya Ulaya ili kuharakisha na kuunganisha taratibu, kuundwa kwa polisi ya mipaka ya Ulaya.

Rais wa Ufaransa pia alitaka kuanzishwa kwa "mshikamano" wa mpango wa mafunzo na ushirikiano wa wakimbizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.