Pata taarifa kuu
EU-WAKIMBIZI-HAKI-USALAMA

Umoja wa Ulaya wapendekeza kupokea wakimbizi 50,000 katika miaka miwili

Tume ya Ulaya inapendekeza mpango mpya wa kupokea wakimbizi katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Wakimbizi hao ni wale kutoka Afrika na Mashariki ya Kati.

EU imeweka mpango wa kupokea wakimbizi 50,000 kutoka Afrika au Mashariki ya Kati.
EU imeweka mpango wa kupokea wakimbizi 50,000 kutoka Afrika au Mashariki ya Kati. REUTERS/Yiannis Kourtoglou
Matangazo ya kibiashara

Mipango iliyowekwa mbele na Tume ya Ulaya inaangazia kuwasili kwa wakimbizi 50,000 katika kipindi cha miaka miwili kama sehemu ya sera mpya ya Ulaya kutoa nafasi kwa wakimbizi kuingia Ulaya.

Mipango ya Ulaya inaangazia tangu miaka miwili iliyopita kupunguza idadi kubwa ya wakimbizi waliowasili tangu majira ya joto mwaka 2015.

Miongoni mwa mipango hiyo ni pamoja na kuwatambua wakimbizi ambao tayari wamewasili katika ardhi ya Ulaya na kuwapokea wakimbizi wanaoelekea kwa wingi Ulaya.

Wakati huo huo, Tume ya Ulaya inapendekeza kuteua mwandamizi wa mpango huo wa kupokea wakimbizi 50,000 wa ziada ifikapo Oktoba 2019.

Bajeti ya Euro nusu bilioni imetangazwa kwa kusaidia kwa hiari nchi za Ulaya kuwapokea wanaotafuta hizi hifadhi.

Maeneo yanayolengwa ni Afrika Kaskazini na Pembe ya Afrika; Tume ya Ulaya inataja hasa Libya, Misri, Niger, Chad, Sudan na Ethiopia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.