Pata taarifa kuu
UFARANSA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji katika kambi ya La Chapelle nchini Ufaransa wahamishwa

Wahamiaji waliokua wakipewa hifadhi katika kambi ya La Chapelle kaskazini mwa mji wa Paris, wameanza kuhamishwa Ijumaa hii Julai 7, 2017, wakati ambapo hali ilikua si nzuri katika sehemu hii ya mji mkuu wa Ufaransa.

Wahamiaji waliopewa hifadhi katika kambi ya La Chapelle, kaskazini mwa mji wa Paris, Juni 29, 2017.
Wahamiaji waliopewa hifadhi katika kambi ya La Chapelle, kaskazini mwa mji wa Paris, Juni 29, 2017. CHRISTOPHE ARCHAMBAULT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Operesheni ilizinduliwa muda mfupi baada ya 6:00 asubuhi saa za Ufaransa. Watu waliohamishwa wametakiwa kupelekwa katika IIe-de-France kwa makazi ya muda.

Operesheni hii kabambe ilizinduliwa mapema asubhui kaskazini mwa mji wa Paris. Wahamiaji kati ya 1000 na 2000 wanatazamiwa kuhamishwa kutoka katika kambi hiyo. Walikuwa wamewekwa karibu na mji wa La Chapelle, kutokana na ukosefu wa uwezo wa malazi na kuongezeka kwa kasi wahamiaji ambao walikua wakiingia kwa wingi katika kipindi cha wiki za hivi karibuni.

Zoezi hili limefanyika kwa utulivu, kwa mujibu wa mwandishi wetu Pierre Olivier, huku barabara kadhaa zikifungwa kwa magari kutokana na zoezi hili la kuwahamisha wahamiaji kwenda Ile-de-France. Mabasi zaidi ya sitini yametumiwa kwa zoezi hili.

Maafisa 350 wa polisi na wafanyaka zi wengine wa serikali wanashiriki zoezi hili, kwa mujibu wa mamlaka.

Wahamiaji waliopewa hifadhi katika kambi ya La Chapelle, kaskazini mwa mji wa Paris, Juni 29, 2017.
Wahamiaji waliopewa hifadhi katika kambi ya La Chapelle, kaskazini mwa mji wa Paris, Juni 29, 2017. CHRISTOPHE ARCHAMBAULT / AFP

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.