Pata taarifa kuu
UFARANSA-ULAYA-SIMONE VEIL

Ufaransa na Ulaya wampoteza Simone Veil, mtu muhimu katika maendeleo ya wanawake

Simone Veil, mtu muhimu na maarufu aliejikubalisha katika maisha yake yote kupambana, katika enzi zake kuhusu hali ya wanawake barani Ulaya alifariki siku ya Ijumaa Juni 30. Rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali nchini Ufaransa na barani Ulaya zimeendelea kutolea kwa familia ndugu zake.

Rais wa zamani wa Bunge la Ulaya Simone Veil wakati wa uzinduzi wa Agora Simone Veil, Brussels mwaka 2011.
Rais wa zamani wa Bunge la Ulaya Simone Veil wakati wa uzinduzi wa Agora Simone Veil, Brussels mwaka 2011. AFP PHOTO / Thierry Charlier
Matangazo ya kibiashara

Simone Veil alikuwa mmoja wa watu muhimu kwa wananchi wa Ufaransa kwa sababu alikua akimpa nasaha mwanae wa kiume Jean Veil, "mfumo wa ujasiri, maadili muhimu." "Hii ni picha ya uzalendo na ya kimaadili" kwa mujibu wa mwanafalsafa Jean d'Ormesson.

Hivi ni vita alivyoendesha ambavyo vilimfanya kuwa maarufu. Ukombozi wa wanawake, bila shaka, lakini pia mapambano yake kwa amani barani Ulaya. Wanasiasa mbalimba nchini Ufaransa wanakaribisha ujasiri wake na kuonyesha umuhimu wake katika siasa ya Ufaransa na Ulaya.

Vigogo wenzake kutoka mrengo wa kati walikua wa kwanza kutoa rambirambi kwa kuunga mkono kazi kubwa alioifanya. Alikuwa "mfano kwa maisha na kwa amani, bila kusahau vita alivyoendesha ili kupatikana kwa yote hayo," alisema Jean-Louis Borloo, kiongozi wa zamani wa UDI, huku akiongeza kwamba Simone Veil alikua "mfano wa karne yetu, mfano wa mwanamke, mfano wa uzuri na mapambano. "

Rais Emmanuel Macron alitoa "rambirambi zake" baada ya kifo cha Simone Veil, akiomba "mfano wake" uweze "kuhamasisha wananchi wenzetu."

Rais wa zamani Nicolas Sarkozy pia alitoa rambirambi zake,akipongeza kwenye Facebook mwanamke "aliyefurahia" na "kupenda" na ambaye "ataendelea kukumbukwa."

Bernard Accoyer, Katibu mkuu wa cham acha Republican amesema "tunapoteza mmoja wa wanawake wakuu wa wakati wetu, mfano wa ujasiri na ubinadamu, alisema kwenye Twitter, huku akiongeza alikuwa mfano, ataendelea kukumbukwa sana kwa vita alivyoendesha. "

Simone Veil aliyechaguliwa rais wa Bunge la Ulaya mwaka 1979, alikuwa pia mfano na mtu muhimu wa Umoja wa Ulaya. "Ujumbe wake bado utabaki kuwa hai kuhusu sheria na jukumu la wanawake barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.