Pata taarifa kuu
UFARANSA-MACRON

Chama cha Rais Macron chaelekea kupata wingi wa viti vya ubunge

Chama cha rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kinaelekea kupata ushindi wa kishindo kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi mkuu wa wabunge uliofanyika mwishoni mwa juma akiviacha kwa mbali vyama vya kitamaduni vilivyozoeleka kwenye bunge la nchi hiyo.

Эмманюэль Бриджит Макрон на избирательном участке в Туке, 11 июня 2017.
Эмманюэль Бриджит Макрон на избирательном участке в Туке, 11 июня 2017. REUTERS/Christophe Petit Tesson/Pool TPX IMAGES OF THE DAY
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya awali yameonesha chama cha Macron cha Republique en Marche kikiongoza sambamba na mshirika wake chama cha MoDem ambapo huenda wakashinda viti ya kati ya 400 hadi 445 katika bunge lenye vnafasi 577.

Ikiwa vyama hivi vitapata ushindi kwenye uchaguzi wa duru ya pili uliopangwa kufanyika Juma lijalo, vitashuhudia vikipata idadi ya viti vinavyotakiwa kwa chama kuwa na uwingi wa viti bungeni tukio ambalo litakuwa halijawahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 60.

Hata hivyo zoezi la upigaji kura liligubikwa na kujitokeza kwa idadi ndugu ya watu walioshiriki kwenye uchaguzi wa safari hii ambao walikuwa ni chini ya asilimia 50 katika kile kinachoonekana kuwa ni mgawanyiko wa siasa za wapinzani wa Macron anayeeleka kushinda.

Chama cha mrengo wa kulia cha Republicane kilichotarajia kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa wabunge baada ya kuanguka vibaya kwenye uchaguzi wa urais kinaelekea kupata viti kati ya 70 hadi 130 huku chama cha Marin Le Pen kikielekea kupata angalau viti 10.

Chama cha aliyekuwa rais wa nchi hiyo Francois Hollande ndicho kinachoonekana kupoteza zaidi kwenye uchaguzi huu ambapo matokeo ya awali yanaonesha kitapoteza viti vyake zaidi ya 200 kilichokuwa kikishikilia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.