Pata taarifa kuu
UINGEREZA-UCHAGUZI

Wananchi wa Uingereza kupiga kura Alhamisi

Wananchi wa Uingereza wanajiandaa kupiga kura siku ya alhamisi kuwachagua wabunge wapya, huku chama kitakachoshinda kikiunda serikali. kulingana na uchunguzi uliofanywa na vyommbo vya habari vya Uingereza, chama cha Waziri Mkuu Theresa May kwa sasa kinaongoza kwa asilimia 41.5 huku Labour ikiwa na aslimia 40.4.

Wakaazi wa mj wa London wakikusanyika kwa kuomboleza vifo vya watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika eneo la Tower Bridge Juni 3, 2017.
Wakaazi wa mj wa London wakikusanyika kwa kuomboleza vifo vya watu waliouawa katika shambulio lililotokea katika eneo la Tower Bridge Juni 3, 2017. REUTERS/Tom Jacobs
Matangazo ya kibiashara

Ushindani mkubwa ni kati ya chama cha Waziri Mkuu Theresa May na kile cha Labour kinachoongozwa na Jeremy Cobin.

Ni uchaguzi unaokuja wakati huu nchi hiyo ikiendelea kukabiliana na hatari ya kushambuliwa na magaidi lakini baada ya kuanza mchakato wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya.

Kura za maoni nchini Uingereza kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Alhamisi wiki hii zinaonesha ushindani mkali kati ya chama tawala Conservative na kile cha kile cha upinzani cha Labour.

Chama cha Waziri Mkuu Theresa May kwa sasa kinaongoza kwa asilimia 41.5 huku Labour ikiwa na aslimia 40.4.

Chama kitakachoshinda idadi kubwa ya viti bungeni kati ya 650 vinavyowaniwa, ndicho kitakachounda serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.