Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI 2017

Uchaguzi Ufaransa 2017: Marin Le Pen katika kashfa nyingine ya matumizi mabaya ya fedha

Mshauri wa zamani wa mgombea uraus nchinij Ufaransa kwa tiketi ya chama cha mrengo wa kulia, Marin Le Pen, ametoa tuhuma dhidi ya kiongozi huyo, safari hii zikihusu udanganyifu mkubwa wa kifedha uliofanywa na chama chake cha Front Nationale, FN.

Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha FN nchini Ufaransa, Marin Le Pen, akihutubia kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni.
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha FN nchini Ufaransa, Marin Le Pen, akihutubia kwenye moja ya mikutano yake ya kampeni. REUTERS/Stephane Mahe
Matangazo ya kibiashara

Gael Nofri amesema kuwa mwaka 2012 chama cha FN, kilimchukua na kumuingiza kwenye timu ya kampeni za urais za Le Pen, ambapo walitumia mkataba wa kufikirika wa bunge la umoja wa Ulaya, hatua iliyolenga chama hicho kukwepa kuweka wazi matumizi ya kwenye kampeni zake.

Chama cha Le Pen tayari kipo chini ya uchunguzi kuhusu tuhuma kuwa kimetumia vibaya fedha za bunge la umoja wa Ulaya.

Kura za maoni zinaonesha kuwa Le Pen anaongoza na huenda akashinda kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais wa mwezi April, lakini mgombea kutoka chama cha msimamo wa kati Emmanuel Macron, ameanza kupata umaarufu na kumkaribia sana Le Pen, kura zikionesha atamshinda kwenye duru ya pili ya uchaguzi huo mwezi April.

Akinukuliwa na moja ya vyombo vya habari nchini Ufaransa, Nofri, amesema kuwa alichukuliwa na chama cha FN mwaka 2011 na kwamba mwaka 2012 aliambia kuna tatizo na kwamba lazima wa tumio njia ya kupitia bunge la umoja wa Ulaya, na hapo ndipo alipolazimika kufanya kazi na mhasibu Nicolas Crochet.

Mtandao mmoja wa habari nchini Ufaransa, umeandika habari za uchunguzi, zikionesha ushahidi wa Euro elfu 3, 834, fedha ambazo yalikuwa malipo ya Nofri kwa mwezi kuanzia mwaka 2012, chama cha FN kikimuanisha kama msaidizi wa Jean-Marie Le Pen, baba mzazi wa Le Pen na kiongozi wa zamani wa chama hicho.

Nofri anasema hakuwahi kuwa msiaidizi wa Jean-Marie Le Pen. Maafisa wengine watatu wa chama hicho wanachunguzwa na polisi akiwemo mlinzi wa Marin Le Pen, Thierry Legier.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.