Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI-SIASA

Kampeni za uchaguzi zaanza nchini Ufaransa

Kampeni za uchaguzi mkuu wa rais nchini Ufaransa zimeanza kurindima mwishoni mwa juma hili wakati huu wagombea nafasi hiyo wakiendelea kutafuta ushawishi kwa ajili ya kuwakilisha mrengo wa kulia na ule wa hushoto katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Marine Le Pen katika mkutano wake mjini Lyon, Februari 5, 2017.
Marine Le Pen katika mkutano wake mjini Lyon, Februari 5, 2017. REUTERS/Robert Pratta
Matangazo ya kibiashara

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wa chama cha National Front, Marine Le Pen ameweka bayana sera yake iwapo atachaguliwa kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Ufaransa ikiwa ni pamoja na kurejesha uhuru wa kitaifa, mapambano dhidi ya Uislam wenye msimamo mkali pamoja na vita dhidii ya uhamiaji haramu. Hata hivyo hajasahau kuwashambulia wapinzani wake.

Upande wake Benoit Hamon ambae amethibitishwa jana na chama chake cha PS kuwania nafasi hiyo baada ya kumpiku waziri mkuu wa zamani Manuel Valls, amesema kubwa kwake ni muungano dhabiti.

Wakati huo huo wagombea Jean Luc Melanchon na Manuel Macron wamenadi pia sera zao kwa wafuasi wao kutafuta uungaji mkono katika uchaguzi huo ambao kampeni zake zimeanza kwa kila mgombea kumshambulia mwingine kwa wakati wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.