Pata taarifa kuu
UFARANSA-SIASA

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kufunguliwa mashtaka

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atafunguliwa mashtaka ya kuvunja sheria ya matumizi ya fedha za kampeni ya siasa wakati wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2012.

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy
Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy GEORGES GOBET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Sarkozy anatuhumiwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha, kinachokadiriwa kuwa Euro Milioni 22.5 na kutoa taarifa za uongo kwa kutumia kampuni ya uhusiano mwema ya  Bygmalion.

Kiongozi huyo wa zamani anatuhumiwa pia alishawishi kampuni hiyo kutoa stakabadhi ya matumizi ya fedha hizo kwa chama chake wakati huo cha UMP, badala ya Kamati kuu ya kampeni.

Jaji Serge Tournaire, ametangaza kuwa kesi hiyo itasikilizwa baada ya kiongozi huyo wa zamani kushindwa kutumia kuzuia kesi hiyo kusikilizwa mwaka uliopita.

Hata hivyo wakili wake Thierry Herzog amesema kuwa mteja wake atakataa rufaa ya kutaka kutofunguliwa mashtaka kuhusu madai hayo.

Sarkozy mwenye umri wa miaka 61, amekuwa akipambana na kesi kadhaaza kisiasa baada ya kupoteza urais mwaka 2012 dhidi ya rais Francois Hollande.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.