Pata taarifa kuu
UFARANSA-FILLON-UCHUNGUZI-HAKI

Mahakama ya Paris kundelea na uchunguzi dhidi Fillon

Mgombea wa urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Republican François Fillon amepata pigo jipya baada ya viongozi wa Mashtaka kusema kuwa hawajasitisha uchunguzi dhidi ya madai ya kumlipa mkewe mshahara wa zaidi ya Euro laki sita kwa kazi ambayo hakuifanya alipokuwa Seneta.

François Fillon, mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais, Februari 15, 2017 katika mji wa Compiègne.
François Fillon, mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais, Februari 15, 2017 katika mji wa Compiègne. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Ofisi ya kiongozi Mashtaka imesema kuwa ushahidi mwingi umeshakusanywa, na sasa ni vigumu sana kuachana na uchunguzi huo.

Fillon amekanusha madai hayo na kusema, yanalenga kumchafulia jina.

Mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa urais alijieleza kwa ufafanuzi zaidi Februari 6, 2017 kuhusu shutuma zilizotolewa dhidi yake, ikiwa ni pamoja na ajira ya mkewe na watoto zake Bungeni.

François Fillon kwanza alisisitiza kuhusu kazi yake ya muda mrefu katika siasa. "Kwa sasa ni miaka 32 sina hofu na vyombo vya sheria, " Bw Fillon alikumbuka.

François Fillon alisema kuwa hana hatia kwa shutuma zinazotolewa. "Nakabiliwa na mashambulizi ya vurugu yasiyokuwa ya kawaida," Bw Fillon alisema akishutumu, huku akihakikisha kwamba kupitia kashfa hizi zinazopeperushwa katika vyombo vya habari, "ni mgombea wa mrengo wa chama cha Republican anayelengwa ".

François Fillon alihakikisha kwamba mambo haya ni "sahihi na yako wazi," akitaja kazi tofauti aliyoifanya mkewe, Penelope. Alieleza kuwa kwa miaka 15, mkewe alipokea mshahara wa wastani wa kila mwezi wa Euro 3677 pesa taslimu.

Lakini mgombea huyo aliomba radhi kwa wananchi wa Ufaransa, na kutambua kuwa alifanya "kosa" kwa kumuajiri mkewe. "Kuna mazoea ya zamani katika siasa, mazoea ambayo hayakubaliki tena," alisema mbele ya waandishi wa habari zaidi ya 200, akimaanisha "ushirikiano wenye uaminifu ambao leo unazua tuhuma."

Hata hivyo alisema hakuna sababu ya kurejesha kiasi cha pesa alichopkea mkewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.