Pata taarifa kuu
UFARANSA-USALAMA

Askari wa Ufaransa ashambuliwa katika makavazi ya Louvre

Mwanjeshi wa Ufaransa anayelinda jengo la kihistoria la makumbusho jijini Paris nchini Ufaransa, amempiga risasi na kumuua mwanaume aliyejaribu kumshambulia askari aliyekuwa anapiga doria.

Maafisa wa Idara ya Dharura na Askari polisi wametumwa karibu na makavazi ya Louvre, Ijumaa hii Februari 3.
Maafisa wa Idara ya Dharura na Askari polisi wametumwa karibu na makavazi ya Louvre, Ijumaa hii Februari 3. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, mwanaume huyo aliyekuwa anatamka Allahu Akbar alijaribu kutekeleza shambulizi hilo kutumia panga.

Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve amesema mwanaume huyo alikuwa analenga kutekeleza shambulizi la kigaidi.

Baada ya jaribio hili, rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa ni lazima kuwa makini kuhusu matukio kama haya.

Trump ametoa matamshi haya siku chache baada ya kuagiza kuzuiwa kwa wakimbizi kutoka mataifa saba za Kiislamu kuja nchini humo.

Ufaransa imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya mwaka uliopita, kushuhudia shambulizi la kigaidi na kusababisha mauaji jijini Paris na Nice.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.