Pata taarifa kuu
HUNGARY-WAKIMBIZI

Mabango ya kupinga kampeni ya serikali dhidi ya wahamiaji

Mamia ya mabango yanayopinga ujumbe wa serikali ya Viktor Orban dhidi ya wahamiaji yameonekana nchini Hungary ili kukabiliana na "kampeni ya hofu" ya serikali, mwezi mmoja tu kabla ya kura ya maoni juu ya kugawana wakimbizi katika Umoja wa Ulaya (EU).

Wahamiaji wakisubiri kuokolewa na maafisa wa uokoaji wa SOS Mediterranean na Madaktari Wasiokuwa na Mipaka, Mei 24, 2016, katika pwani ya Libya.
Wahamiaji wakisubiri kuokolewa na maafisa wa uokoaji wa SOS Mediterranean na Madaktari Wasiokuwa na Mipaka, Mei 24, 2016, katika pwani ya Libya. GABRIEL BOUYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunapinga hali yoyote ya kukuza chuki iliyobuniwa na serikali hii," amesema Jumanne hii Septemba 6 Gergo Kovacs, kutoka chama cha MKKP - Magyar Kétfarkú Kutya, chama ambacho kwa miaka kadhaa kinapambana dhidi ya kauli na hotuba mbovy za Waziri Mkuu Viktor Orban.

Katika majira haya ya joto, serikali imezindua kwenye vyombo vya habari kampeni mpya dhidi ya wahamiaji. "Je, unajua hayo? Zaidi ya watu 300 wamefariki barani Ulaya tangu mwanzo wa wimbi la wahamiaji "; "Ubelgiji inataka tupokea idadi ya wahamiaji sawa na ukubwa wa mji"; "Wakimbizi milioni wanasubiri kuja Ulaya".

"Kampeni ya Hofu"

Baadhi ya raia wa Hungary wanapinga mpango huo wa serikali, huku wakijaribu kujibu kwa mabango 800 na maelfu ya nyaraka zinazopinga hotuba hiyo: "Je, unafahamu hilo? Watu si wajinga "; "Je, unafahamu hilo? Zaidi ya raia milioni moja kutoka Hungary wanataka kuondoka Hungary kwenda Ulaya "; "Je, unafahamu hilo? Kuna vita nchini Syria. "

Kovacs ameshutumu "kampeni ya hofu" wakati inakaribia kura ya maoni, iliyopangwa kufanyika Oktoba 2, wakati ambapo Viktor Orban, anapinga kanuni ya kugawana wakimbizi katika nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya, huku akiwatolea wito raia wa Hungary kupiga kura kwa kuunga mkono au kupinga utaratibu huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.