Pata taarifa kuu
ITALI-JANGA

Watu wasiopungua 120 wafariki kwa tetemeko la ardhi Italia

Watu wasiopungua 120 wamefariki kutokana na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 kwenye vipimo vya Richter lililotokea saa zamwanzo mapema Jumatano hii katika eneo la kati la milima nchini Italia, kilomita 140 kaskazini mwa mji wa Roma.

Tetemeko la ardhi lasababisha hasara kubwa katika mji wa Amatrice, mji mdogo katikati mwa Italia.
Tetemeko la ardhi lasababisha hasara kubwa katika mji wa Amatrice, mji mdogo katikati mwa Italia. REUTERS/Remo Casilli
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Italia, Matteo Renzi, amesema zaidi ya watu 120 wamefariki kutokana na tetemeko la ardhi lililopiga Italia Jumatano hii.

Maelfu ya wakazi wa eneo hilo hawana makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa na tetemeko hilo la ardhi. Watu wengine wengi wamefukiwa chini ya vifusi.

Wengi wamefafiki katika kijiji cha Pescara del Tronto ambacho kimeharibiwa vibaya na inahofiwa kwamba idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.

Tetemeko hilo la ardhi limeshuhudiwa katika miji ya Umbria, Latium na Marches. Wilaya zilizoathirika zaidi ni Accumoli, Amatrice, Posta na Arquata del Tronto.

Mitetemeko ilisikika katika miji ya mbali kama vile Roma, Venice, Bologna na Naples. Mjini Roma, baadhi ya majumba yalitikisika kwa sekunde 20, kwa mujibu wa gazeti la La Repubblica.

Mji wa Amatrice nao pia uliharibiwa vibaya. Watu wanne wanahofiwa kufariki katika mji jirani wa Accumoli.

Kitovu cha tetemeko hilo la ardhi kimemekuwa karibu na mji wa Norcia, mji wa kitalii katika eneo la Umbria, kwenye kina cha urefu wa kilomita 4, ambapo inaelezwa kwamba uharibifu ulikua mkubwa.

Ufaransa imependekeza kutoa msaada kwa Italia, Ikulu ya Elysee imetangaza, na kusikitika kwamba "janga hilo ni la kutisha." Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye yuko ziarani Tallinn katika mkoa wa Estonia, pia ametangaza kuwa nchi yake iko tayari kutoa msaada unaohitajika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.