Pata taarifa kuu
UBELGIJI-MASHAMBULIZI-UGAIDI

Ubelgiji: utata kuhusu mshukiwa mkuu wa mashambulizi ya Brussels

Ousama Atar, raia wa Ubelgiji, mwenye umri wa miaka 32, ni mmoja wa watu wanaotafutwa nchini Ubelgiji. Ousama Atar binamu wa magaidi wawili waliojilipua Machi 22 katika mji wa Brussels, ni mshukiwa mkuu wa mashambulizi hayo.

Heshima ya mwisho yatolewa kwa wahanga wa mashambulizi ya mjini Brussels katika Kasri la Mfalme Philip na Malkia Mathilde.
Heshima ya mwisho yatolewa kwa wahanga wa mashambulizi ya mjini Brussels katika Kasri la Mfalme Philip na Malkia Mathilde. REUTERS/Eric Vidal
Matangazo ya kibiashara

Jumanne hii Agosti 16, Ousama Atar amezusha utata nchini ubelgiji. Mtuhumiwa huyo aliachiwa huru kwa ombi la serikali ya Ubelgiji mwaka 2012 wakati ambapo alikua akizuiliwa nchini Iraq.

Oussama Atar, kwa sasa anasakwa na polisi ya Ubelgiji. Mwaka 2004 alihukumiwa kifungo cha miaka 10 jela nchini Iraq kwa kosa la kutokua na kibali kinachomruhusu kuishi katika nchi hiyo wakati ambapo alikua akivuka mpaka wa Syria.

Mwaka 2010, familia yake ilianzisha utaratibu wa kumuondoa kutoka jela, wakibaini kwamba anakabiliwa na saratani ya figo. Maandamano yalifanyika nchini Ubelgiji, kwa msaada wa shirika la la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International na Wabunge kadhaa. Ousama Atar hatimaye alifanikiwa katika kesi yake. Aliachiliwa huru mwaka 2012 kwa ombi la Wizara ya Mambo ya Nje kwa sababu za kiafya.

Utata

Kuachiliwa kwa Ousama Atar kumezusha leo utata: Mbunge Alain Destexhe ameomba ufunguzi wa uchunguzi kuhusu jukumu la shirika la haki za binadamu la Amnesty International na Wabunge waliohusika. "Amnesty International iliweza kusaidiwa mtu huyo hatari kuachiwa huru, mtu ambaye tayari alikua mwenye msimamo mkali wa kidini," amesema Bw Destexhe. Amnesty inajitetea na kubaini kwamba walifanya maandamano kwa ajili ya haki ya kupewa huduma za kimatibabu wala si kuachiwa huru.

Wiki iliyopita, wajumbe watatu wa familia ya Ousama Atar, ikiwa ni pamoja na mama yake, walihijiwa kisha wakaruhusiwa kurudi nyumbani. Muhusika huyo mkuu wa mashambulizi ya Machi 22, bado ni hajakamatwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.