Pata taarifa kuu
EU-UINGEREZA

Waasisi wa Umoja wa Ulaya waitaka Uingereza kujiondoa haraka iwezekanavyo

Mataifa yaliyo asisi muungano wa Ulaya EU, yanaitaka Uingereza kuanza kuondoka katika muungano huo"haraka iwezekanavyo" ili kuiondoa jumuiya hiyo katika mkwamo, waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani amesema leo Jumamosi.

Mawaziri wa mataifa sita muhimu yaliyoasisi muungano wa Ulaya  katika mkutano jijini Berlin Ujerumani 25/06 2016
Mawaziri wa mataifa sita muhimu yaliyoasisi muungano wa Ulaya katika mkutano jijini Berlin Ujerumani 25/06 2016 REUTERS/Axel Schmidt
Matangazo ya kibiashara

Frank-Walter Steinmeier, akiongoza mkutano wa mataifa sita yaliyo asisi Muungano wa Ulaya jijini Berlin, amesema wako katika makubaliano kwamba Uingereza haitakiwi kusubiri utaratibu mgumu wa kujiondoa katika muungano huo.

Hayo yanajiri baada ya kura ya maoni ya siku ya Alhamisi kuhusu Uingereza kubaki ama kujitoa ndani ya Umoja wa Ulaya ambapo asilimia 52 ya wapigakura waliunga mkono kujiondoa.

Kufuatia kura hiyo Thamani ya sarafu ya Uingereza, Sterling pound imeshuka kwa kiwango kikubwa mno kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30 iliyopita.

Aidha baada ya matokeo ya kura ya maoni yaliyoshtusha bara la Ulaya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na raisi wa Ufaransa Francois Hollande walitoa muongozo wa wito kwa Umoja wa Ulaya kufanya mageuzi ili muungano huo uweze kustahimili baada ya Uingereza kujiondoa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.