Pata taarifa kuu
UHAMIAJI-ULAYA

Wahamiaji: watu zaidi ya 21 wapoteza maisha katika bahari ya Aegean

Watu wasiopungua 21, wakiwemo watoto wanane, wamekufa maji baada ya boti mbili walizokuwemo kuzama Ijumaa hii asubuhi katika pwani ya visiwa vya Farmakonisi na Kalolimnos katika bahari ya Aegean. Wahamiaji wengine kadhaa hawajulikani walipo, polisi ya bandari ya Ugiriki imesema.

Wahamiaji wakiwasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos, baada ya kuvuka Bahari ya Aegean kutoka Uturuki, Septemba 10, 2015.
Wahamiaji wakiwasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos, baada ya kuvuka Bahari ya Aegean kutoka Uturuki, Septemba 10, 2015. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

Walinzi wa pwani wamekua wakiendelea kuwatafuta asubuhi hii wakati ambapo idadi halisi ya watu waliokosekana haijajulikana hadi sasa, lakini inaweza kuwa na inaweza kufiki mamia kulingana na ushahidi uliyotolewa na manusura waliokwenda upande wa pwani ya Uturuki, chanzo cha polisi kimebaini. Kwa ujumla, watu 74 waliokolewa.

Baada ya ajali ya boti la kwanza iliyotokea karibu saa 6:30 saa za kimataifa, usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, miili ya watoto sita na mwanamke mmoja imeokolewa na walinzi wa pwani. Watu 48 waliookolewa katika pwani ya Farmakonissi hawakupata jeraha lolote na afya yao inaendelea.

Masaa kadhaa baadaye, boti jingine imezama katika kisiwa kidogo cha Kalolimnos na polisi wa bandarini waliokoa miili 14 mapema asubuhi. Watoto Miili ya watu hao iliookolewa ni pamoja na watoto wawili, wanawake tisa na wanaume watatu, polisi imetangaza.

Kwa jumla watu 26wamenusurika katika ajali hii ya pili . Wamearifu kwamba watu wengi walikua katika boti hilo. Polisi ya bandarini inaendelea na zoezi la kutafuta miili mingineambayo bado haijapatikana.

Alhamisi wiki hii, wahamiaji wasiopungua 12, wakiwemo watoto, walikufa maji katika pwani ya magharibi ya Uturuki baada ya boti waliokuwemo kuzama. Boti hilo lilikua likijaribu kuingia katika visiwa vya Ugiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.