Pata taarifa kuu
ULAYA-WAKIMBIZI

Wahamiaji milioni moja waingia Ulaya mwaka 2015

Wahamiaji milioni moja wameingia Ulaya mwaka huu, idadi ambayo ni kubwa tangu Vita vikuu ya pili vya dunia, Umoja wa Mataifa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) wamesema, wakibaini pia kwamba wahamiaji walingia kwa kiasi kikubwa tangu mwezi Oktoba.

Wahamiaji wakiwasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos baada ya kupitia Uturuki, Septemba 4, 2015.
Wahamiaji wakiwasili katika kisiwa cha Ugiriki cha Lesbos baada ya kupitia Uturuki, Septemba 4, 2015. AFP/AFP/
Matangazo ya kibiashara

"Desemba 21, watu 972,000 walivuka bahari ya Mediterranean, kulingana na takwimu za Shirika la kimataifa linalohudumia wakimbizi (HCR). Aidha, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) linabaini kwamba zaidi ya wakimbizi na wahamiaji 34,000 waliingia nchini Bulgaria na Ugiriki baada ya kupitia Uturuki", IOM na HCR zimesema katika taarifa ya pamoja.

Walioingia kwa njia ya bahari mwaka huu walikuwa wengi karibu mara tano ikilinganishwa na mwaka 2014.

Hili ni "wimbi kubwa la wahamiaji tangu Vita vikuu vya pili vya dunia" barani Ulaya, IOM imesema katika taarifa yake nyingine iliyotumwa kwa vyombo vya habari.

Mwaka 2015, kwa mujibu wa HCR na IOM, "idadi ya watu waliovuka bahari ya Mediterranean iliongezeka kwa kasi, kutoka 5,000 mwezi Januari hadi kufikia zaidi ya 221,000 mwezi Oktoba."

Tangu wakati huo, idadi hiyo imepungua. Wahamiaji na wakimbizi 67,700 waliingia nchini Ugiriki wakipitia katika bahari mwezi Desemba, kwa mujibu wa IOM. Kupungua huko kulitokana na hali mbaya ya hewa na kukandamizwa kwa wapita njia na viongozi wa Uturuki, kwa mujibu wa taasisi hizo mbili za kibinadamu zenye makao yao mjini Geneva.

Idadi kubwa ya wakimbizi na wahamiaji - zaidi ya 821,000 - walipitia Ugiriki, 816,000 kati yao walipitia kwa bahari.

Aidha, takriban wakimbizi na wahamiaji 150,000 wameingia tangu mwezi Januari nchini Italia, karibu 30,000 nchini Bulgaria, zaidi ya 3,800 nchini Uhispania, 269 nchini Cyprus na 106 nchini Malta, kwa mujibu wa shirika moja lenye makao yake mjini Geneva.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.