Pata taarifa kuu
AUSTRIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wakimbizi: Hungary yafunga mpaka wake

Mataifa ya Umoja wa Ulaya (EU), yameshindwa Jumatatu wiki hii kuafikiana juu ya mgawanyo wa wakimbizi, baada ya nchi kadhaa kuanzisha mfumo wa ukaguzi kwenye mipaka na Hungary kuamua kufunga mpaka wake na Serbia.

Jeshi la Hungary limetamatisha zoezi la kuweka uzio, Septemba 14, 2015 katika mpaka na Serbia.
Jeshi la Hungary limetamatisha zoezi la kuweka uzio, Septemba 14, 2015 katika mpaka na Serbia. ATTILA KISBENEDEK/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji wakiangusha kilio mbele ya nyaya walizowekewa ghafla mbele yao: Budapest imeamua kufunga Jumatatu mpaka wake na Serbia wakati ambapo nchi za Ulaya zikikutana Brussels, kujaribu kutafutia suluhu suala la wimbi la wakimbizi linalotishia uhuru wa kutembea barani Ulaya.

Katika mji wa Röszke, eneo kuu wanakopitia wahamiaji kwenye mpaka wa Serbia, askari polisi kumi na tano wa Hungary wakivalia sare ya bluu wamekua wakiwazuia wakimbizi kupita eneo hilo, wakati ambapo maafisa wengine wakiweka nyaya za kwenye barabara, kwa mujibu wa waandishi wa habari wa AFP.

Wahamiaji waliowasili eneo hilo wakitokea Serbiawamekua wakiangsha walipoona barabara ikifungwa. Na kuanzia siku ya Jumanne wiki hii, Hungary itatekeleza sheria mpya ya kutoruhusu wakimbizi kupitia kwenye mpaka wake.

Wakati huo huo, mjini Brussels, waziri wa mambo ya nje wa Luxembourg, Jean Asselborn, amewaonya viongozi wa Ulaya.

" Kama hatuafikiani kwa pamoja leo, Ulaya itasambaratika ", ameonya Bw Asselborn, ambaye ameongoza kikao dharura cha baraza la mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya.

Mawaziri hawa waliotafautiana, walikua wakijadili hatua ziliyopendekezwa wiki iliyopita na Tume ya Ulaya, ambayo ilitoa wito kwa Mataifa wanachama kugawana, kwa mujibu wa sheria idadi sawa ya wakimbizi 160,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.