Pata taarifa kuu
UTURUKI-PKK-MASHAMBULIZI-USALAMA

Uturuki yaendelea kupambana na makundi yenye silaha

Kundi la waasi la DHKP-C la mrengo wa kuchoto limekiri kuhusika na shambulio dhidi ya ubaozi mdogo wa Marekani katika mji wa Istanbul, nchini Uturuki, huku kundi lingine la waasi wa mrengo wa kushoto la HSB, likikiri kuhusika na shambulio dhidi ya kituo cha polisi.

Mpiganaji wa kundi moja la mrengo wa kushoto akiwa katika mtaa mmoja wa Istanbul, katika mazishi ya mmoja wa waathirika wa mabomu ya Suruç.
Mpiganaji wa kundi moja la mrengo wa kushoto akiwa katika mtaa mmoja wa Istanbul, katika mazishi ya mmoja wa waathirika wa mabomu ya Suruç. AFP PHOTO /YASIN AKGUL
Matangazo ya kibiashara

Kundi hili la HSB lililionekana kwa mara ya kwanza kuanzisha harakati zake mwezi Machi mwaka 2014 wakati wa shambulio dhidi ya gazeti lililo karibu na kundi la Islamic State. Tangu wakati huo kundi hili halikurudi kusikika. Kundi lina nadharia ya kundi, "Marxist Leninist Maoist" lenye mafungamano na kundi dogo la Tikko, jeshi la ukombozi wa wafanyakazi na wakulima wadogo wadogo wa Uturuki.

Haijajulikana hata kidogo malengo ya kundi hili, ispokua tu lina uhusiano wa kiitikadi wa karibu nakundi la DHKP-C ambalo limedai kuhusika na shambulio dhidi ya ubalozi mdogo wa Marekani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, Istanbul, Jérôme Bastion, mrendo wa kushoto unaona kuwa serikali ya Uturuki ina uhusiano upande mmoja na Waislam wenye msimamo mkali. Makundi hayo yenye silaha ya mrengo wa kushoto yameahidi kuzilenga pande hizi mbili ( serikali ya Ututuruki na makundi ya waislam wenye msimamo mkali). msimamo huo pia umekua ukitumiwa na kundi la HPG, ambalo ni tawi la kijeshi la kundi la wa waasi wa Kikurdi la PKK, ambalo kwa muda fulani, limekua likiendesha mashambulizi kwa watu mashuhuri katika uislam au watuhumiwa wa kundi la Islamic State katika mji wa Istanbul.

Makundi haya ya mrengo wa kushoto yanahisi kutishiwa na waislam wenye msimamo mkali pamoja na serikali ya Uturuki, ambapo yametanza vita. Hali hii inatisha, na huenda ikasababisha kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kundi la [DHKP-C] limekuwepo tangu miaka ya 1970. Kuliwahi kutokea nchini Uturuki aina ya vita vya kiraia kati ya mrengo wa kushoto na mrengo wa kulia. Kundi hili lilikua tangu zamani lenye msimamo mkali. Lakini baadae lilitoweka, lakini iwapo limeanzisha tena harakati zake ni kutokana huenda na serikali ya Uturuki imekua ikiwashambulia Wakurdi wa Syria, ikishirikiana na Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.