Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Ugiriki: hatua kuelekea kumaliza mgogoro

Marais na viongizi wa serikali 19 wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro wamehitimisha mkutano wao katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels jumatatu jioni wiki hii.

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras baada ya mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro kuhusu Ugiriki, mkutano uliyofanyika Brussels, Juni 22 mwaka 2015.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras baada ya mkutano wa kilele wa viongozi wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro kuhusu Ugiriki, mkutano uliyofanyika Brussels, Juni 22 mwaka 2015. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Mapendekezo ya maelewano yaliyotolewa na Ugiriki yalikaribishwa na wakopeshaji wake wa kimataifa na nchi nyingine 18 zinazotumia sarafu ya Euro. Makubaliano hayajakamilika lakini sasa wanaonekana kuwa wako tayari kukubaliana wakati mabapo Ugiriki inapaswa kulilipa shirika la fedha IMF Euro bilioni 16 ifikapo Juni 30. Inaonekana kuwa Ugiriki haiwezi kulipa deni hilo kwa tarehe hiyo iliyopangwa kama haitopata msaada wa kimataifa.

Kwa mara ya kwanza tangu karibu miezi minne yalipoanza mazungumzo, mapendekezo ya mageuzi yaliyofanywa na Ugiriki, nchi za Ulaya zimeona kuwa yanatosha na misingi ya makubaliano yamewekwa pamoja wakati huu, kulingana na kauli ya rais wa Ufaransa François Hollande na rais wa Tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker.

Jean-Claude Juncker amesisitiza kuwa mapendekezo ya Ugiriki " yamepiga hatua kubwa " kuelekea taasisi za mikopo na amesema ana imani kwamba wiki hii watafikia mkataba wa jumla.

Kiongozi mkuu wa kundi la Umoja wa Ulaya, Jeroen Dijsselbloem, amesema kwamba ombi la hivi karibuni la Ugiriki limefanya msingi mzuri wa mpango wa misaada ya kifedha na mahitaji ya haraka ya Athens.

Waziri wa uchumi wa Ugiriki Giorgios Stathakis amesema kwamba ombi la hivi karibuni pamoja na ongezeko la ushuru katika masuala ya biashara na utajiri ni wakati ambapo juhudi zinafanywa kuepusha zoezi linaloendelea la ukataji mafao ya wafanyakazi kutoka katika mishahara yao.

Wataalam wana siku mbili kwa kuhesabu athari ya kifedha ya mapendekezo yaliyotolewa na Ugiriki. Hesabu hii itawasilishwa Jumatano jioni wiki hii kwa mawaziri wa fedha 19 wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro. Nakala ya mkataba wa mwisho inaweza hatimaye kupitishwa na marais pamoja na viongozi wa serikali katika mkutano ujao unaotazamiwa kufanyika siku ya Alhamisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.