Pata taarifa kuu
UGIRIKI-ULAYA-UCHUMI

Tsipras, Merkel na Hollande wakutana kando ya mkutano wa EU-CELAC

Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras alikutana Jumatano wiki hii na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa François Hollande, kando ya mkutano wa kilele kati ya Umoja wa Ulaya na nchi za Amerika Kusini na Caribbean, mjini Brussels.

Angela Merkel, Alexis Tsipras, Hollande wameongea kwa karibu masaa mawili kando ya mkutano wa kilele wa EU-CELAC.
Angela Merkel, Alexis Tsipras, Hollande wameongea kwa karibu masaa mawili kando ya mkutano wa kilele wa EU-CELAC. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao walikubaliana "kuimarisha" juhudi ili kufungulia majadiliano na hatimaye kufikia makubaliano kati ya Athens na taasisi zinazoidai.

Kwa karibu masaa mawili ya mazungumzo, François Hollande, Angela Merkel na Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras walichukua muda wa kushughulikia hali ngumu inayoikabili Ugiriki, ambayo inaweza kuwa katika tatizo kubwa la kutekeleza ahadi yake ya malipo mwishoni mwa mwezi huu kama hakuna ufumbuzi unapatikana.

Mazungumzo ya kisiasa, wala si ya kiufundi, ambayo yalifanyika katika hali nzuri, kwa mujibu wa Kansela wa Ujerumani. Francois Hollande na Angela Merkel kwa mara nyingine walirejelea kwamba mkataba unapaswa kwanza kufikiwa na taasisi tatu, pande tatu zinazodai Ugiriki ambazo ni Umoja wa Ulaya, Benki kuu ya Ulaya na Shirika la Fedha Duniani.

Ufumbuzi utatoondokana na majadiliano ambayo yanaendeshwa na Ugiriki na pande hizo tatu. Francois Hollande na Angela Merkel waliweza kukubaliana kuzieleweza pande hizo tatu zinazodai Ugiriki wiki iliyopita mjini Berlin. Ugiriki inapaswa skutoa mapendekezo yanayokubalika ikiwa ni pamoja na VAT, pensheni au mageuzi ya kimuundo. Mapendekezo ambayo yatapaswa kutangazwa kwa haraka ili kuepuka kutotekeleza malipo ambayo yanaweza kudhoofisha nchi zinazo tumia sarafu ya Euro.

Mgogoro huu pia unaathiri uchumi wa nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya. Leo Alhamisi, Waziri mkuu Ugiriki atakutana tena na rais wa Tume ya Ulaya, Jean-Claude Juncker. Itakuwa, pengine, nafasi ya kutangaza hatimaye mapendekezo ambayo yatapelekea kuondokana na mgogoro huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.