Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-RISHWA-SHERIA

Chuck Blazer atumiwa kwa kufichua kashfa za rushwa FIFA

Kashfa za rushwa zinazoelezwa kwa kiasi kikubwa katika Shirikisho la Kandanda Duniani FIFA, ziliyotolewa Jumatano asubuhi wiki hii baada ya kukamatwa kwa maofisa saba wa Shirikisho hilo, ni za muda mrefu.

Chuck Blazer alikuwa mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA wakati alikuwa akifanya udukuzuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia Fifa kwa kipindi cha miaka miwili.
Chuck Blazer alikuwa mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA wakati alikuwa akifanya udukuzuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia Fifa kwa kipindi cha miaka miwili. AFP PHOTO / PETER KOHALMI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, yote yalianza mwaka 2011, wakati Idara ya uchunguzi ya Marekani (FBI) ilifaulu kumshawishi Chuck Blazer kuwa afisa wake wa ujasusi. Chuck Blazer alikuwa mwanachama wa kamati tendaji ya FIFA tangu mwaka 1998 hadi mwaka 2013. Chuck Blazer alilitumikia Shirikisho la Concacaf, ambalo ni sawa ni Shirikisho la Soka Duniani FIFA.

Chuck Blazer alikuwa akifanya udukuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia FIFA kwa kipindi cha miaka miwili. Alikubali kuwafanyia kazi viongozi wa Marekani baada ya kugunduliwa na mamlaka ya kodi kwa kushindwa kulipa kodi kwa mamilioni ya fedha aliyopitisha mlango wa nyuma kwa kipindi cha miaka ishirini na moja akiwa kama Katibu mkuu mtendaji wa Concacaf, ambalo ni Shirikisho la Soka la Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean.

Kati ya mwaka 2011 na 2013, wakati alikua bado mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA, Chuck Blazer alikua akibebelea chombo kidogo cha kurekodi sauti ambaco alikua akikificha kwenye funguo zake gari. Chuck Blazer alirekodi mazungumzo zaidi ya mia moja, ambayo yote yaliwekwa kwenye faili iliyofunguliwa na Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Mashariki ya New York, Loretta Lynch, ambaye ni waziri wa sheria wa Marekani tangu Aprili 27.

Kwa sasa, maofisa tisa wa FIFA waliochaguliwa pamoja na wadau watano wa uongozi wa soka wameshtakiwa rasmi kwa tuhuma za kashfa ya rushwa, hasa kuhusiana na utoaji wa Kombe za Dunia, haki za masoko na televisheni. Jambo ambalo limezua hali ya sintofahamu, kwani Ijumaa wiki hii kutafanyika uchaguzi wa rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA. Uchaguzi utafanyika wakati ambapo rais wa sasa wa FIFA, Sepp Blatter, raia wa Uswisi anayemaliza muda wake, ambaye amekua akikosolewa mno, anatazamiwa kuwania muhula wa tano. Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA limeomba uchaguzi huu uahirishwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.