Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-SHERIA

Kandanda: maofisa kadhaa wa Fifa wakamatwa Uswisi

Jumatano Mei 27, maofisa kadhaa wa Shirikisho la soka duniani Fifa wamekamatwa na polisi katika hoteli moja ya kifahari katika mji wa Zurich, nchini Uswisi.

Rais wa shirikisho la Soka duniani Fifa, Joseph Blatter.
Rais wa shirikisho la Soka duniani Fifa, Joseph Blatter. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watu hawa wanatuhumiwa na mahakama ya Marekani kwa kashfa za rushwa ziliyofanywa katika miaka ishirini iliyopita.

Kwa mujibu wa ofisi ya shirikisho la mahakama ya Uswisi, maafisa sita wa soka ndio waliokamatwa mapema Jumatano asubuhi.

Taarifa hii ya kukamtwa kwa maofisa hawa wa Fifa imetangazwa na gazeti la New York Times. Maofisa hao wamekamatwa katika hoteli moja ya kifahari ya Zurich, iliyo karibu na makao makuu ya Shirikisho la Soka duniani Fifa.

Vyombo vya sheria vya Marekani vimeomba watu hao watumwe Marekani wahojiwe kwa makosa wanaotuhumiwa ambayo yanahusiana na kashfa ya rushwa, ikiwa ni pamoja na mikataba ya masoko, lakini pia hali ya utoaji wa Kombe za Dunia vikombe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.