Pata taarifa kuu
UFARANSA-ARGENTINA-AJALI-USALAMA

Ajali ya helikopta Argentina : Uchunguzi waanzishwa

Uchunguzi kuhusu ajali ya helikopta mbili iliyogharimu maisha ya watu kumi ikiwa ni pamoja na wanamichezo watatu wa Ufaransa nchini Arentina, umeanzishwa, siku saa chache baada ya tukio hilo kutokea.

Wachunguzi wamekua na kazi ngumu ya kupata dalili katika eneo la Villa Castelli, katika mkoa wa La Rioja, kulikotokea ajali ya helikopta mbili, ajali ambayo iligharimu maisha ya watu 10, Machi 10 mwaka 2015.
Wachunguzi wamekua na kazi ngumu ya kupata dalili katika eneo la Villa Castelli, katika mkoa wa La Rioja, kulikotokea ajali ya helikopta mbili, ajali ambayo iligharimu maisha ya watu 10, Machi 10 mwaka 2015. REUTERS/Jorge Torres
Matangazo ya kibiashara

Afisa anayehusika na uchunguzi amekusanya miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo ambao walikua wakishiriki katika kutengeza makala ya mchezo wa kusisimua ya “télé-réalité” inayorushwa kwenye runiga ya Ufaransa TF1.

Wahusika wakuu wapepigwa na mshutuko baada ya kutokea kwa ajali hiyo. Kitengo cha kisaikolojia kimewekwa ili kusaidia kupata njia kwa uchunguzi unaoendelea. Pamoja na hilo, kinachohitajika ni kwenda mbele ya vyombo vya sheria vya Argentina, ambavyo kupitia ushahidi wao, vinataka kufafanua masuala mengi yanayozunguka tukio hili.

Uchunguzi utaweka wazi iwapo ajali hii ilisababishwa na hitilafu ya uendeshwaji au tatizo la kiufundi. Lakini tayari, picha za kugongana kwa helikopta hizo , ajali iliyogharimu maisha ya wanamichezo watatu wa Ufaransa na watu wengine saba, zinaonesha baadhi ya vitu ambavyo vinaweza kutumiwa kwa uchunguzi huo ambao umeanzishwa.

Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na Florence Arthaud, Camille Muffat bingwa wa michezo ya kuogelea ya olimpiki na mwanamisumbi Alexis Vastine.

Mabingwa hao watatu wamekua wakishiriki pamoja na wanariadha wengine wa Ufaransa katika utengenezaji wa makala ya " télé-réalité", ambayo ni mchezo mpya wa kusisimua wa televisheni ya Ufaransa TF1.

Watu wote hao kumi waliofariki walikua katika helikopta mbili walizokua wakitumia katika kazi yao hio, ambazo ziligongana, kwa mujibu wa viongozi wa mkoa wa La Rioja.

Inaarifiwa kua helikopta hizo ziligongana baada ya kuruka kwenda juu kwenye umbali wa mita 100. Picha za ajali hiyo zinatisha.

Saa moja baadae, polisi ya moka wa La Rioja ilitoa taafa kwamba hakuna mtu aliyenusurika katika ajali hiyo. Marubani wawili kutoka Argentina wote wamefariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.