Pata taarifa kuu
UFARANSA-UGAIDI-Maandamano

Kibonzo cha Mtume Muhammad kwenye toleo la wiki hii

Jarida linalochapisha vibonzo mjini Paris nchini Ufaransa Charlie Hebdo limesema katika toleo lake la hapo kesho siku ya Jumatano litachapisha kibonzo cha Mtume Muhammad katika ukurasa wa mbele, akiwa na bango lenye maandishi “Je suis Charlie”, ikimaanisha “mimi ni charlie nimesamehe yote”.

Mkutano wa kwanza wa waandishi wa habari  walionusurika wa jarida la vibonzo la Charlie Hebdo baada ya mauaji, Januari 9, mwaka 2015.
Mkutano wa kwanza wa waandishi wa habari walionusurika wa jarida la vibonzo la Charlie Hebdo baada ya mauaji, Januari 9, mwaka 2015. AFP PHOTO / BERTRAND GUAY
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mashambulizi ya kigaidi mwanzoni mwa mwezi Januari nchini Ufaransa, ambayo yaligharimu maisha ya watu 17, wakiwemo wachoraji maarufu wa jarida la kila wiki la Charilie Hebdo, rais wa Ufaransa amechukua uamzi wa kuimarisha usalama katika maeneo mbalimbali.

Takribani wanajeshi 10,000 wametumwa nchi nzima kwa muda usiyojulikana, hususan katika shule za Wayahudi pamoja na maeneo ya ibada kwa Waislam. Idadi ya askari polisi imeongezwa.

Akizungumza siku moja baada ya maandamano makubwa ya umma nchini Ufaransa kuwahi kutokea , kwa heshima ya wahanga , Waziri wa ulinzi Jean-Yves Le Drian amesema nchi hiyo bado iko katika hatari ya mashambulizi zaidi.

Wakati hiuo huo miili ya wayahudi wanne waliouawa mjini Paris wakati wa shambulizi dhidi ya jarida linalochapisha vibonzo mjini Paris Nchini ufaransa imesafirishwa asubuhi hii mjini Jerusalem huko Israeli kwa ajili ya mazishi, wizara ya mambo ya nje ya Israel Imebainisha.

Mauaji ya Raia hao wanne kutoka Israel yalizusha masikitiko makubwa miongoni mwa wananchi wa Israel waishio jijini Paris nchini Ufaransa, ambao wengi baadhi yao ni wamiliki wa maduka na majengo ya kifahari jijini humo.

Akizungumza kupitia televisheni inayomilikiwa na serikali ya Israel mjini Jerushalem, msemaji wa serikali alifahamisha kuwa raia hao wanne wayahudi waliouawa huko Paris ni Yoav Hattab, Philippe Braham, Yohan Cohen naFrançois-Michel Saada nao waliuawa katika shambulizi katika soko la kosher linalouza vyakula vya Kiyahudi, mashariki mwa mji mkuu wa Ufaransa Paris, tukio lililosababisha watu kadhaa kujeruhiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.