Pata taarifa kuu
IS-Marekani, Ufaransa, Iraq, Syria-Usalama

IS yatoa vitisho dhidi ya Marekani na Ufaransa

Wapiganaji wa Dola la Kiislam wametolea wito waislam kuuwa raia hususan kutoka Marekani na Ufaransa, nchi ambazo zinaunda muungano wa kimataifa uliyoanzishwa kwa minajili ya kupambana dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam walioko nchini Iraq na Syria.

Wapiganaji wa kikurdi "peshmerga" wakiwa katika uwanja wa mapigano dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, nchini Iraq. Agosti 18 mwaka 2014.
Wapiganaji wa kikurdi "peshmerga" wakiwa katika uwanja wa mapigano dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislam, nchini Iraq. Agosti 18 mwaka 2014. REUTERS/Youssef Boudlal
Matangazo ya kibiashara

“ Iwapo utaweza kumuua raia asiyokua na imanai ya dini kutoka Marekani au barani Ulaya, hususan ufaransa, Australia, au Canada, au raia wowote kutoka mataifa yanayoshiriki katika muungano wa kimataifa dhidi ya Dola la Kiislam, kwa hiyo mtumainiye Mungu na umuuwe kwa aina yoyote”, msemaji wa Dola hilo la Kiislam, Mohammed al-Adnani, ametangaza kwa lugha tofauti.

Ujumbe huo uliyorekodiwa kwa lugha ya kiarabu ukiwa na tafsiri ya maandishi kwa kingereza, kifaransa na kiebrania, umetoa mfano wa jinsi gani kitendo hicho cha kuua kinapaswa kutekelezwa, bila hata hivo kubebelea silaha za jeshi, wakitoa mfano wa kuchinja, kuchoma kwa kutumia kisu au kutumia sumu.

Marekani na Ufaransa ni nchi mbili ambazo hadi sasa zimeendesha mashambulizi ya anga nchini Iraq dhidi ya ngome za wapiganaji wa Dola la Kiislam.

Wapiganaji wa Dola la Kiislam wamejiuliza iwapo Marekani haina uwezo wa kupambana ardhini.

Msemaji wa dola la Kiislamu amelipongeza kundi la watu wenye silaha wanaoendesha harakati zake katika eneo la Sinai nchini Misri, akiwatolea wito kuwakata vichwa wanaounga mkono utawala wa rais Abdela Fattah Al Sisi.

Wakati huo huo Tume ya Umoja wa Ulaya imeimarisha ulinzi kwenye majengo yake dhidi ya visho vya wapiganaji wa Dola la Kiislam, baada ya wapiganaji hao kutoa taarifa vitisho dhidi ya mataifa yanayounda muungano wa kimataifa dhidi ya Dola la Kiislam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.