Pata taarifa kuu
EU-URUSI-UKRAINE-Usalama

Ubelgiji: Ukraine: mataifa ya Ulaya yatiwa hofu na mwenendo wa Urusi

Mawaziri wa mambo yanje wa nchi za Ulaya wanaokutana katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels, wameiyonya Urusi dhidi ya kuingilia kijeshi nchi ya Ukraine, baada ya taarifa zinazosema kwamba vifaru na magari ya jeshi la Urusi yameingia nchini Ukraine. 

Viongozi wa mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatiwa wasi wasi na hali inayoendelea nchini Ukraine.
Viongozi wa mataifa 28 wanachama wa Umoja wa Ulaya wanatiwa wasi wasi na hali inayoendelea nchini Ukraine. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

“Ninatiwa wasi wasi na taarifa zinazosema kwmba vifaru na magari ya jeshi la Ukraine yameingia nchini Ukraine. Iwapo kuna magari aidha wanajeshi wa Urusi nchini Ukraine, wanapaswa kuondoka haraka iwezekanavyo, la sivyo hali itakua ngumu zaidi”, amesema wazairi wa Uingereza mwenye dhamana ya mambo ya nje Philip Hammond.

Hammond amesema hayo kabla ya serikali ya Kiev kuthibitisha kwamba wanajeshi wa Urusi wamevuka mpaka na kuingia nchini Ukraine, wakipitia katika eneo linaloshikiliwa na waasi mashariki mwa taifa hilo, baada ya kufahamishwa na wanahabari wa Uingereza.

“Hali hii inatia wasi wasi”, ameongeza Hammond.

“Huu ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa”, amesema waziri wa mambo ya nje wa Sweden, Carl Bildt.

Kawa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Denmark, Martin Lidegaar, ameelezea wasi wasi wake juu ya mwenendo wa Urusi wa hivi karibuni, hasa kitendo hiki cha kuingiza wanajeshi wake nchini Ukraine.

“viongozi wa Urusi wanapaswa kuwa makini kwa Umoja wa Ulaya hata Marekani ,kwani tumeamua kujibu kwa muda wowote iwapo Urusi itashambulia kijeshi Ukraine”, amesema Lidegaar.

Mawaziri hao wa mambo ya nje wa Ulaya wanakutana katika kikao cha dharura ili kuonesha ungwaji wao mkono kwa raia wa Iraq wanaopigana dhidi ya wapiganaji wa ISIL, na kutathimini hali inayoendea nchini Ukraine.

Hayo yakijiri, rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea kwa mazunguzo rais wa Finland, Sauli Niinistö, moja ya nchi za Ulaya inayoathirika kutokana na kuongezeka kwa mzozo kati ya Moscow na mataifa ya magharibi.

“Nimekuja kuzunguza uwezekano wa kupatia ufumbuzi machafuko yanayoendelea nchini Ukraine (...) kutazama jinsi ya kila mmoja kutoa mchango wake ili hali ya utulivu irejeuye katika taifa hilo”,amesema rais Niinistö, kabla ya kukutana kwa mazungumzo na rais wa Urusi katika ikulu yake mjini Sotchi, kusini mwa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.