Pata taarifa kuu
Croatia

Raia wa Croatia waishio nje ya nchi yao waanza kupiga kura

Wananchi wa croatia waishio nje ya nchi yao, wameanza zoezi la kupiga kura ya uchaguzi wa bunge utaofanyika nchini Croasia kesho jumapili, ambapo matokeo ya uchaguzi huo ndio yatasababisha kupatikana kwa serikali itayo endesha juhudi za nchi hiyo kujiunga na umoja wa ulaya mwaka 2013.

Wagombea wa uchaguzi wa ubunge nchini Croatia
Wagombea wa uchaguzi wa ubunge nchini Croatia
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa mapema asubuhi saa kumi na mbili katika nchi hamsini na vinafungwa jioni saa kumi na mbili, imearifu radio ya taifa ya nchi hiyo.

Takriban wapigakura lakini nne na elfu kumi na moja raia wa Croasia wanaoeshi ugenini ndio wataopiga kura, huku wapigakura laki mbili na elfu sitini na nne wakiwa nchini Bosnia, jirani na Croasia ambako vituo zaidi ya thalathini vilifunguliwa.

Hata hivyo wananchi wa Croasia waishio ugenini watawachaguwa wabunge watatu kati ya wabunge mia moja hamsini na moja wataounda bunge la nchi hiyo.

Kampeni ya uchaguzi ilihitimishwa jana katika mji wa Zagreb, ambapo kesho jumapili wananchi wapatao milioni moja onusu watawachaguwa wabunge kwa muhula mwingine wa miaka minne.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.