Pata taarifa kuu
ITALIA - CROATIA

Papa Benedict wa XVI kufanya ziara ya kwanza ya kihistoria nchini Croatia

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedict wa XVI leo anatarajia kuanza ziara ya siku mbili nchini Croatia  moja ya nchi katika mataifa ya ulaya yenye waumi wengi zaidi wa kanisa hilo. 

Papa Benedict wa XVI
Papa Benedict wa XVI REUTERS/Tony Gentile
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Vatican Federico Lombardi amesema kuwa Papa antarajia kukutana na viongozi wa nchi hiyo ambapo baadae atahutubia katika ziara ambayo wacahmabuzi wa masuala ya dini wanasema kuwa inaumuhimu mkubwa kwa taifa hilo.

Ziara hiyo inakuwa ya kwanza ya kihistoria kufanywa na Papa Bendict wa XVI tangu kuteuliwa kwake ambapo amekuwa mstari wa mbele kuipigania nchi hiyo kuweza kupatiwa uanachama wa kudmu wa umoja wa ulaya.

Licha ya kiongozi huyo kuwa mstari wa mbele kuipigania nchi hiyo kupewa uanachama wa umoja wa ulaya, bado wananchi wa taifa hilo wameonyesha wasiwasi wao endapo nchi hiyo itajiunga na umoja huo kuwa itapoteza utambulisho wake wa taifa pamoja na utamaduni wa watu wa nchi hiyo.

Nchi ya Croatia ni moja kati ya mataifa ya ulaya ambayo yamekuwa yakiongozwa kwa misingi ya kidini hususani ya katoliki ambapo mara kadhaa wananchi wamekuwa wakiandamana kupinga nchi yao kujiunga na umoja huo.

Hata hivyo Papa Benedict mara kadhaa amewataka wananchi wa taifa hilo kutokuwa na wasiwasi kuhusu nchi yao kujiunga na umoja huo akisema kuwa kuwemo katika umoja wa ulaya kutasaidia nchi hiyo kukua kiuchumi na kueongeza ushirikiano na mataifa ya ulaya katika sekta mbalimbali.

Siku ya jumapili kiongozi huyo anatarajiwa kutembelea eneo maalumu la kiongiozi wa zamani wa kanisa katoliki aliyeiongoza kanisa hilo wakati wa vita ya pili ya dunia, huku kukiwa na ukososaji mkubwa wa sehemu ya kumbukumbu ya kiongozi huyo ambaye anashutumiwa kuwa alishirikiana na utawala wa kinazi wakati wa vita ya pili ya dunia.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.