Pata taarifa kuu
AU-UHURU-MAENDELEO

Umoja wa Afrika kujadili masuala yanayoukabili

Mawaziri wa mambo ya nje kutoka mataifa ya Afrika, wanakutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, kueleka Mkutano mkuu wa viongozi wa matafa ya Afrika.

Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Moussa Faki Mahamat, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. JOHN THYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Suala kuu bila shaka ni kuhusu kujitegemea kwa Umoja wa Afrika ambapo kwa kiasi kikubwa mahitaji makuu ya Umoja huo hufadhiliwa na washirika wa Umoja wa Ulaya, Japan na China, bila uwepo wa uhuru. Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat amesema Umoja wa Afrika ukiwa huru unawezakusonga mbele na kujitegemea zaidi katika nyanja mbalimbali.

Lakini baadhi ya mataifa ya Afrika yanasita kutoza kodi ya asilimia 0.2 ya bidhaa zao. Rais mtarajiwa wa Umoja wa Afrika, Paul Kagame, anataraji kueleza Jumapili hii ni hatua gani ambazo zitachukuliwa kwa nchi hizo na marekebisho ambayo yatafikia makubaliano na kuthibitishwa na nchi zote zinazounda umoja huo.

Suala jingine ambalo litajadiliwa ni kuhusu uhamiaji ambalo lilijadiliwa miezi miwili iliopita katika kiako cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Ulaya kilichofanyika mjini Abidjan nchini Cote d’Ivoire baada ya kusambaa kwa mkanda wa video ulioonyesha soko la wahamiaji wakiuzwa kama watumwa nchini Libya.

Desemba 6 mwaka jana, Umoja wa Afrika ulitangaza kuwa utawaondoa wahamiaji elfu ishirini waliokwama nchini Libya katika kipindi cha majuma sita yajayo. Lakini leo majuma hayo yamekwisha, hakuna kilichotekelezwa. Katika uzinduzi wa mkutano wa mawaziri wa Umoja wa Afrika jana Alahamisi, Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Mussa Faki Mahamat na Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea, Mamady Toure, hawakuzungumzia lolote kuhusu hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.