Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MADURO-USALAMA-SIASA

Rais Maduro atoa wito kwa mazungumzo na upinzani

Rais wa Venezula Nicolas Maduro anasema yuko tayari kuzungumza na upinzani nchini humo ili kumaliza mzozo wa kisiasa unaoendelea.

rais wa Venezuela, Nicolás Maduroaomba mazungumzo na upinzani.
rais wa Venezuela, Nicolás Maduroaomba mazungumzo na upinzani. Fuente: Reuters.
Matangazo ya kibiashara

Upinzani ambao umepanga maandamano makubw hivi leo, kwa wiki tatu sasa mawlfu ya wafuasi wa uoinzani wamekuwa wakiandamana kote nchini kushinikiza rais Maduro ajiuzulu na kuitisha Uchaguzi mpya haraka iwezekanavyo kwa kile wanachosema ni dikteta.

Venezuela imeendelea kukumbwa na maandamano ambapo kwa wiki iliyopita pekee raia wa nchi hiyo waliandamana siku mbili mfululizo wakidai rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro ajiuzulu.

Waandamanaji zaidi ya 20 walipoteza maisha katika makabiliano na maafisa wa usalama.

Kwa miezi kadhaa, muungano wa upinzani MUD, ulio na idadi kubwa ya wabunge nchini humo, umeendelea na harakati zake katika katika mchakato wa kura ya maoni dhidi ya Rais Nicolas Maduro. Hatua ya kwanza ilisahihishwa mapema mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.