Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAANDAMANO-USALAMA

Upinzani Venezuela kuingia tena mitaani

Upinzani nchini Venezuela umepanga kuandamana tena Alhamisi hii Aprili 20. jana Jumatano maelfu ya raia wa Venezuela wameandamana katika mji mkuu wa Caracas na katika miji mingine zaidi ya 20.

Maelfu ya  raia wa Venezuela wameandamana katika mji mkuu wa Caracas na katika miji mingine zaidi ya 20
Maelfu ya raia wa Venezuela wameandamana katika mji mkuu wa Caracas na katika miji mingine zaidi ya 20 REUTERS/Christian Veron
Matangazo ya kibiashara

Katika maandamao ya jana waandamanaji walipandamana mitaani wengine wakimuunga mkono rais Nicolas Maduro na wengine wakiipinga serikali.

Kiongozi mkuu wa upinzani Henrique Capriles amezungumza na waandishi wa habari kuwa siku ya leo watakutana raia wote wa Venezuela wakiwa na lengo la kushinikiza rais Maduro kuondoka madarakani.

Waandamanaji wanataka kufanyike uchaguzi wa Urais na kuachiliwa huru kwa wanasiasa wa upinzani.
Polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wapinzani mjini Caracas, ambapo kijana mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi.

Katika mji wa magharibi mwa nchi hyo San Cristobal, mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya maandamano kugeuka vurugu.

Hata hivyo Rais Maduro ameulaumu upinzani kwa kusababisha vurugu.

Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, Venezuela imeendelea kukumbwa na mfumuko mkubwa wa bei, visa vingi vya uhalifu na uhaba wa bidhaa muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.