Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Rais Kabila asema kuhuzunishwa na matukio ya Septemba 19 na 20

Katika ujumbe wa Ofisi ya rais uliosomwa kwenye redio na televisheni vya taifa, RTNC, Joseph Kabila amesema anaamini kwamba maandamano ya amani yaliyokua yaliandaliwa "yaligeuzwa na waandaaji, kwa kuwa vurugu makabiliano yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa."

Rais wa DRC, Joseph Kabila, ambaye amesema hakuna kitakachozuia kufanyika kwa uchaguzi.
Rais wa DRC, Joseph Kabila, ambaye amesema hakuna kitakachozuia kufanyika kwa uchaguzi. DR
Matangazo ya kibiashara

Rais Joseph Kabila amelinganisha hali hiyo na ile iliyotokea katika mji wa Kinshasa mwaka 1991 na 1993. "Matumizi ya uasi hayawezi kamwe kuwa njia mbadala kwa mazungumzo," amesema Rais Joseph kabila. Katika tangazo hili, Rais Kabila ametoa wito kwa mara nyingine kwa wale wote ambao bado wanasita kujiunga na wengine katika mjadala wa kitaifa uliyosimamishwa hadi Ijumaa wiki hii, kushiriki katika mazungumzo hayo haraka iwezekanavyo.

Rais Joseph Kabila ametoa rambirambi zake kwa familia za wahanga na hasa "askari polisi wa taifa waliouawa na kujeruhiwa katika wakiwa katika majukumu yao ya kila siku ambayo ni kuimarisha usalama wa taifa, " Rais kabila amebaini.

Hayo yakijiri baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamekusanyika katika makundi madogo Jumatano hii katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa. Idadi ya askari polisi ambao walikua wengi katika mji wa Kinshasa ilizuia waandamanaji kuandamana kwa wingi baada ya siku mbili za maandamano yaliyosababisha vifo vya 44 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Mashahidi na wakazi wa mji wa Kinshasa wamesema kwamba hali ya imerejea kuwa ya kawaida katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Lakini matukio kadhaa yameshuhudiwa katika baadhi ya maeneo. Marundo ya matairi yamechomwa moto na polisi walifaulu kuwatimua waandamanaji kwa kufyatua risasi hewani.

Maandamano yalianza Jumatatu wiki hii kwa wito wa muungano wa upinzani wa ambao unamshtumu Joseph Kabila kutaka kusalia madarakani licha ya kupunguza idadi ya mihula ya rais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.