Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Wapinzani waandamana kwa makundi madogo mjini Kinshasa

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani wamekusanyika katika makundi madogo Jumatano hii katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa. Idadi ya askari polisi ambao walikua wengi katika mji wa Kinshasa ilizuia waandamanaji kuandamana kwa wingi baada ya siku mbili za maandamano yaliyosababisha vifo vya 44 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano mjini Kinshasa, Septemba 19, 2016.
Wafuasi wa upinzani wakati wa maandamano mjini Kinshasa, Septemba 19, 2016. AFP/EDUARDO SOTERAS
Matangazo ya kibiashara

Mashahidi na wakazi wa mji wa Kinshasa wamesema kwamba hali ya imerejea kuwa ya kawaida katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Lakini matukio kadhaa yameshuhudiwa katika baadhi ya maeneo. Marundo ya matairi yamechomwa moto na polisi walifaulu kuwatimua waandamanaji kwa kufyatua risasi hewani.

Maandamano yalianza Jumatatu wiki hii kwa wito wa muungano wa upinzani wa ambao unamshtumu Joseph Kabila kutaka kusalia madarakani licha ya kupunguza idadi ya mihula ya rais.

Maandamano hayo yaligubikwa na makabiliano kati ya waandamanaji na polisi. Kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch, watu 44 waliuawa katika ghasia hizo. Hata hivyo serikali ilitangaza kwamba watu 17 ndio waliuawa katika vurugu hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.