Pata taarifa kuu
DRC-MAZUNGUMZO

Kanisa Katoliki lajiondoa katika mazungumzo

Katika taarifa yake Jumanne hii, Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kwamba imesimamisha ushiriki wake katika mjadala wa kitaifa, kwa minajili ya "kuomboleza" baada ya machafuko yaliyosababisha vifo vya watu wengi mjini Kinshasa Jumatatu wiki hii.

Bango linalotoa wito kwa mazungumzo yaliyoitishwa na Rais Joseph Kabila katika mji wa Kinshasa, DRC.
Bango linalotoa wito kwa mazungumzo yaliyoitishwa na Rais Joseph Kabila katika mji wa Kinshasa, DRC. RFI/Habibou Bangré
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waandaaji wa mazungumzo hayo, mazungumzo yanaweza kuendelea Ijumaa, Septemba 23.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, watu 17 ikiwa ni pamoja na askari polisi watatu waliuawa wakati wa maandamano ya Jumatatu wiki hii.

Watu wengine wawili waliuawa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne hii katika makao makuu ya chama cha UDPS, chama kikuu cha upinzani, ambapo kiongozi wake, Etienne Tshisekedi, amesusia kushiriki katika "mazungumzo ya kitaifa".

Makao makuu ya chama cha UDPS cha Etienne Tshisekedi, DRC.
Makao makuu ya chama cha UDPS cha Etienne Tshisekedi, DRC. RFI/Habibou Bangré

Mazungumzo ya kisiasa yanayoendeshwa na mwakilishi wa Umoja wa Afrika, Waziri Mkuu wa zamani wa Togo Edem Kodjo, yanapania kuiondoa DR Congo katika mgogoro unaoendelea kutokota.

Miezi mitatu kabla yakumalizika kwa muhula wa pili wa Rais Joseph Kabila, kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais hakuepukiki, kwa mujibu wa serikali na vyama vinavyoiunga mkono.

Serikali na washirika wake wametoa sababu za kiufundi.

Kambi moja ya upinzani inataka uchaguzi wa urais ufanyike kabla ya mwisho wa mwaka.

Wanashutumu "ujanja" wa Rais Kabila, anayelenga kupitia "mjadala wa kitaifa" kukaa madarakani hata baada ya kumalizika kwa muhula wake wa pili mwezi Novemba.

Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amewatolea wito viongozi wa kisiasa nchini DR Congo kutatua tofauti zao "kwa amani" na "kwa njia ya mazungumzo."

Wakati huo huo Umoja wa Ulaya unatarajiwa kujadiliana kuhusu uwezekano wa kuiwekea vikwazo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Waziri wa mashauriano ya kigeni wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault amesema, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

Marekani tayari imetishia kuwawekea vikwazo baadhi ya wanasiasa kwa kuchelewesha kufanyika kwa uchaguzi, unaotarajiwa mwezi Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.