Pata taarifa kuu
GABON-SIASA

Waziri wa Sheria, Séraphin Moundounga, atangaza kujiuzulu

Waziri wa Sheria wa Gabon Seraphim Moundounga ametangaza Jumatatu hii mchana kwenye vyombo vya habari mjini Libreville, uamuzi wake wa kujiuzulu. Taarifa ambayo imethibitishwa na Waziri huyo kwa RFI.

Séraphin Moundounga, Waziri wa Sheria wa Gabon. (Hapa ni mwezi Juni 2015 mjini Libreville).
Séraphin Moundounga, Waziri wa Sheria wa Gabon. (Hapa ni mwezi Juni 2015 mjini Libreville). Flickr cc
Matangazo ya kibiashara

"Baada ya kuona kwamba upande wa utawala, hawakutoa jibu kuhusu wasiwasi wa muhimu wa kupatikana kwa amani na kuendeleza demokrasia, nimeamua kuchukua uamuzi wa kuchukua likizo, upande mmoja, katika chama cha Democratic Party, na kuachana na majukumu yangu kama mjumbe wa serikali na hasa kuachana na vitendo hivi vikuu viwili, ili niweze kuwa huru kwa shughuli zagnu za kila siku. "

Hayo yakijiri Ufaransa imesema "haina taarifa yoyote kuhusu waliko raia wake" baada ya machafuko makubwa yaliyofuata tangazo la kuchaguliwa kwa mara nyingine tena kwa Rais Ali Bongo nchini Gabon, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Marc Ayrault, amesema Jumatatu hii katika taarifa yake.

"Watu wengi wamekua wakikamatwa katika siku za hivi karibuni. Ufaransa haina taarifa yoyote kuhusu waliko raia wake, " amesema Waziri, ambaye ameonyesha" wasiwasi wake mkubwa". Watu kadhaa, wenye uraia wa nchi mbili Ufaransa na Gabon hawajulikani walipo, chanzo cha kidiplomasia kumeliambia shirika la habari la AFP.

Vurugu zilizuka nchini Gabon baada ya kutangazwa kuwa Ali Bongo Ondimba ameshinda uchaguzi wa urais uliyofanyika wiki moja iliyopita. Upinzani umeendelea kupinga matokeo yaliyotangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani yanayompa ushindi Ali Bongo Ondimba.

Upinzani umeendelea kudai kuhesabiwa upya kwa kura katika vituo vyote vya kura vya mkoa wa Haut-Ogooué, ambako inadhaniwa kuwa kura ziliibwa.

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi huu, Balozi wa New Zealand Gerard van Bohemen, aliwatolea wito "wagombea wote, wafuasi wao, vyama vya siasa na wadau wengine kuwa watulivu, kukomesha vurugu au uchochezi wowote na kutatua migogoro ya aina yoyote kwa njia ya utaratibu wa kisheria na kikatiba. "

Machafuko nchini Gabon yamesababisha vifo vya watu zaidi ya saba na wengine wengi wamekamatwa na wengine hawajulikani waliko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.